Tembo
wanne, (pichani), leo Mei 9, 2017, wameonekana kwenye mazingira ya Chuo
Kikuu cha Dodoma (UDOM), na kuleta tafrani kubwa miongoni mwa
wanafunzi na jumuiya nzima ya chuo. Hata hivyo wataalamu wamesema, Tembo
hao ambao hawakuleta madhara yoyote, "walikuwa safarini", kwani eneo
walikokuwa wakipita ni nia yao ya asili au shoroba na Tembo husifika kwa
kutunza kumbukumbu kama njia aliipita miaka 50 iliyopita anaweza
kurudia palepale na inawezekana ndilo lililotokea leo hii. Askari wa
Mamlaka ya Wanyamapori walifika kwenye eneo hilo na kuchukua tahadhari
kwa kuwaadhibiti ili wasilete madhara kwa wananchi.
Pages
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment