Kampuni za Yapi Merkezi ya Uturuki
na Mota Engil ya Ureno zimewataka Wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi
nchini kutengeneza bidhaa zenye ubora ili kampuni hizo ziweze kutumia
katika Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Standard Gauge (SGR) unayotarajiwa kuanza kujengwa nchini.
Hayo yamesemwa leo na Meneja wa
Mradi huo Mhandisi Maizo Mgedzi katika mahojiano ya ana kwa ana na Idara
ya Habari – MAELEZO Ofisini kwake kwenye makutano barabara ya Reli na
Sokoine Jijini Dar-es-salaam.
Kwa mujibu wa Gazeti la Monitor
la nchini Uganda, likimkariri Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni hivi
karibuni kuhusiana na ujenzi wa SGR, limesema kuwa bei elekezi ya tani
moja ya Saruji kwa fedha za Kitanzania ni Shiingi Laki Tatu (300,000/=)
sawa na Dola za Kimarekani 100, wakati kiasi hicho hicho cha Tani za
Saruji nchini uganda zinauzwa fedha za Uganda Laki Sita (600,000/=) sawa
na Dola za Kimarekani 180.
Aidha, gazeti hilo limeeleza
kwamba, bei ya Nondo tani moja zinazotengeneza nchini Tanzania
inanunuliwa kwa Shilingi milioni 2.4, sawa na dola za Kimarekani 680
ambapo Tani moja ya Nondo nchini Uganda inauzwa kwa fedha za Uganda
Shilingi Milioni 2.47 sawa na Dola za Kimarekani 700.
Kwa mujibu wa Mhandisi wa Mradi
huo nchini Maizo Mgedzi, kutokana na bei elekezi ya ununuzi wa nondo na
saruji kwa ajili ya ujenzi wa reli hiyo muhimu kwa uchumi wa Tanzania,
ni dhahiri Makampuni ya ujenzi wa reli hiyo yatalazimika kununua bidhaa
hizo kutoka hapa nchini, jambo ambalo wazalishaji wanatakiwa kutengeneza
katika kiwango bora kinachotakiwa.
Kutokana na hali hiyo, Mhandisi
Mgedzi amesema, kwa Wazalishaji ambao ni waaminifu watakaoweza
kutengeneza bidhaa zilizo bora, Kampuni hizo mbili za ujenzi kutoka
Ureno na Uturuki zitanunua kwa wingi zaidi ili kuweza kukamilisha ujenzi
wa reli hiyo.
Aidha, kutokana na mahitaji
makubwa ya bidhaa hizo Wazalishaji hao watalazimika kuongeza uzalishaji
huku Kampuni hizo zikiajiri nguvu kazi kubwa ya vijana katika ujenzi wa
reli hiyo ya SGR. Amesema Mgedzi.
Mhandisi Mgedzi amewasihi
Wazalishaji wa bidhaa hizo wahakikishe wanafuata masharti ya Mkandarasi
na Washirika wao kutoka Korea ili kujenga uaminifu na imani kwa
Watanzania kuwa wanao uwezo wa kuzalisha bidhaa bora zaidi na kuondoa
malalamiko na wasiwasi kwa baadhi ya Makandarasi wanaofanya kazi za
ujenzi hapa nchini.
Kinyume na hapo kama watakuwepo
wafanyabiashara wasio na nia njema watajipenyeza na kuleta bidhaa na
vifaa visivyo na ubora, maana yake reli itakayojengwa itakuwa haina
ubora na matokeo yake Serikali ya Tanzania itapata hasara na
haitaikubaliana na matokeo hayo. Amesema Mgedzi.
Akitoa maelezo ya ujenzi wa reli
hiyo Mhandisi Mgedzi amesema utahusisha kumimina nguzo za chini za zege
ambazo zitahitaji mchanga, kokoto , saruji na nondo bora kabisa ili
kuifanya reli kuwa madhubuti na imara.
Kuhusu ujenzi wa Vituo vya reli
hiyo Mdandisi Mgedzi amesema “Vituo vitakavyojengwa vitakuwa tofauti na
vituo vya Reli ya Kati kwa sababu vinahitaji kuwa na njia nyingi zaidi
katika kila kituo kimoja”.
“Hii itarahisisha treni kuweza
kubadilisha njia na pia kukata mabehewa kwa urahisi hususani kwa yale
yanayotakiwa kubaki kituoni na mengine yaweze kuondoka bila kuzuiliwa.
Hivyo, vituo vya reli hii vitahitaji eneo kubwa zaidi katika kila kituo
ukilinganisha na eneo lililopo katika vituo vya reli ya kati”.
Ujenzi wa reli ya SGR ulizinduliwa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
tarehe 12 Aprili, 2017 katika Stesheni ya Pugu. Aidha, Rais aliwaahidi
wakazi wa Pugu kupewa kipaumbele katika kuajiriwa na kufanya kazi wakati
ujenzi wa reli hiyo utakapoanza.
Serikali imewapa Wakandarasi
walioshinda Zabuni ya ujenzi wa reli hiyo miezi 30 kuweza kukamilisha na
kuikabidhi Serikali ya Tanzania. Awamu ya kwanza ya ujenzi huo itaanzia
mji Mkuu wa Biashara wa Dar-es-salaam hadi Morogoro wenye urefu wa
kilometa 205 na itakamilika mwaka 2019. Ujenzi wa reli hiyo utagharimu
fedha za Marekani Bilioni 1.2, sawa na fedha za Tanzania shilingi
Trilioni 2.7 Asilimia 50 ya fedha hizo ni za ndani na Asilimia 50 ni
mkopo kutoka nje.
Tanzania ni nchi ya nne Barani
Afrika kujenga reli ya SGR inayoendeshwa kwa umeme, mafuta au gesi. Nchi
zenye reli kama hiyo ni Ethiopia, Afrika ya Kusini na au Misri
Botwana.
Mradi
wa Ujenzi wa reli hiyo una Washauri Elekezi waliobobea ambao ni Korea’s
national railway operator Korail katika awamu ya kwanza ya ujenzi
Dar-es-salaam – Morogoro. Washauri Elekezi wengine ni M/S Dong Myeong
Engineering Consult, Architecture
LTD, M/S Unitec Civil Consultatnt LTD-Tanzania, M/S Multi-Tech
Consultants (PTY) LTD-Botswana, M/S SSF Incentelre AG-Germany, M/S
D’Appolonia SPA-Italy na M/S Balaji RailroadSystes PrivateLTD-India.
Reli hiyo pia itajengwa kuanzia
Dar-es-salaam hadi Mwanza, kaskazini magharibi mwa Tanzania yenye urefu
wa kilometa 2561 ambayo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mwaka 2019.
Reli hiyo pia inatajaiwa kujengwa hadi Mpanda ikitokea Tabora na Kigoma
pembezoni mwa Ziwa Tanganyika.
No comments :
Post a Comment