Profesa Honest Prosper Ngowi akiwaelekeza baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe kuhusu utafiti unaoangazia masuala ya kodi. Kulia ni Profesa Arne Wiig akitoa maelekezo kwa mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho. Utafiti huo unafanywa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Christian Michelsen Institute (CMI) ya Norway na Chuo Kikuu Mzumbe cha nchini Tanzania. |
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe wakiendelea na utafiti huo jijini Dar es Salaam jana.
NA MWANDISHI WETU
Dar
es Salaam, Tanzania. Wanafunzi wa Mzumbe Dar Es Salaam wakifanya
shughuli za utafiti kwa vitendo katika mradi wa utafiti wa mambo ya
kodi. Mradi huu ni ushirikiano kati ya taasisi ya Christian Michelsen
Institute (CMI) ya Norway na Chuo Kikuu Mzumbe. Unafadhiliwa na Baraza
la Utafiti la serikali ya Norway na upo katika mwaka wa mwisho katika
miaka yake mitatu. Professor Ngowi wa Mzumbe ni mtafiti mkuu katika
mradi huu Tanzania. Watafiti kutoka Norway waliokuwepo Mzumbe ni Prof.
Odd Fjeldstad na Prof. Arne Wiig. Katika utafiti huu wanafunzi walijibu
maswali mbalimbali yahusuyo kodi. Matokeo yake yatatumika kushauri
mamlaka kuhusu mambo kadhaa ya kodi Tanzania. Utafiti wa aina hii
unafanyika pia Angola na Zambia.
No comments :
Post a Comment