WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa,
ameondoka nchini leo Mei 10, 2017 kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa siku mbili wa “Transform
Africa Summit 2017” ulioanza leo Mei 10, 2017 mjini Kigali, Rwanda.
Taarifa kutoka ofisi yake zimesema mkutano huo utawakutanisha viongozi na
wataalam mbalimbali barani Afrika kwa lengo la kujadili masuala kadhaa ikiwemo
maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT), hususan katika ukanda
wa Afrika Mashariki.
Katika
mkutano huo,
Profesa Mbarawa ataeleza kwa kina changamoto na mafanikio yaliyofikiwa
na
Tanzania katika uwekezaji wa Miundombinu ya Habari na Mawasiliano,
Maendeleo ya
Sera na Miongozo inayotumika hapa nchini katika kusimamia sekta hiyo kwa
lengo
la kukuza uchumi wa nchi na kuiunganisha Tanzania na Mataifa mengine.
pichani chini Rais wa Rwanda, Paul Kagame akifungua mkutano huo ambao
ulikwenda sambamba na maonesho ya kiteknolojia.
|
Rais wa Rwanda Paul Kagame, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa “Transform
Africa Summit 2017” ulioanza leo Mei 10, 2017 mjini Kigali, Rwanda. |
|
Washiriki wa mkutano huo wakisikiliza hotuba ya Rais Kagame wakati wa ufunguzi leo |
No comments :
Post a Comment