Friday, May 19, 2017

PENZI LAMFANYA PRINCESS MAKO WA JAPAN KUACHIA HADHI YA KIFALME

Mwanafamilia wa familia ya kifalme ya Japan, Princess Mako, ataachia hadhi ya ufalme, kutokana na kuamua koolewa na mwanaume anayetoka kwenye koo isiyo ya kifalme.

Princess Mako, 25, ambaye ni mjukuu wa Mfalme Akihito ataolewa na mfanyakazi wa kampuni ya sheria aitwaye Kei Komuro mwenye miaka 25 pia ambaye alikutana naye masomoni.

Japan inasheria kali zinazomtaka mwanafamilia wa kifalme wa kike kuondoka katika familia ya Kifalme baada ya kuolewa na mwanaume kutoka kwenye familia isiyo ya kifalme.
                                                     Kei Komuro mwanaume anayemuoa Princess Mako

No comments :

Post a Comment