MAHAKAMA Kuu ya Mtwara imejiwekea malengo ya kumaliza mlundikano wa kesi ifikapo Julai, mwaka huu.
Akitoa taarifa ya Kanda kwa Jaji
Kiongozi- Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali, Jaji
Mfawidhi-Mahakama Kuu-Kanda ya Mtwara Mhe. Fauz Twaib amesema mpaka
kufikia mwezi Aprili, Kanda yake ilikuwa na jumla ya kesi 370 zilizobaki
Mahakamani.
Akifafanua, Jaji Twaib alisema
jumla ya kesi 116 zilisajiliwa kati ya mwezi Januari na Aprili mwaka huu
na kesi 117 zilisikilizwa na kumalizika. Kesi 371 ni zile zilizobaki
Desemba, 2016.
Aidha; kati ya kesi hizo, kesi
288 ni zile zenye umri wa miaka miwili na pungufu mahakamani, kesi 82
zina umri wa miaka mitatu (3) mpaka nne (4) Mahakamani wakati hakuna
kesi iliyozidi miaka mitano (5) Mahakamani.
Amesema Kanda yake ni miongoni
mwa Kanda zilizopatiwa fedha za kuendesha vikao vya kumaliza mlundikano
wa kesihivyo wamefanya vikao viwili (2) Mtwara na Lindi.
Jaji Mfawidhi huyo amesema kikao
cha Mtwara kimepangiwa kusikiliza kesi 32 za madai na ardhi wakati kikao
cha Lindi kinasikiliza kesi nyingine tisa (9) na vikao hivi
vitamalizika Juni 9, mwaka huu.
Jaji Kiongozi-Mahakama Kuu ya
Tanzania yuko kwenye ziara ya kukagua shughuli za Mahakama na kusisitiza
utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania katika Kanda ya
Mtwara inayojumuisha Mikoa ya Lindi na Mtwara.
No comments :
Post a Comment