Mkuu wa jeshi la polisi Nchini
(IGP),Simon sirro aksisitiza jambo wakati alipozungumza na waandishi
habari (hawapo pichani) juu ya hatua mbalimbali za kuweza kudhibiti
masuala ya uhalifu likiwemo la mauaji yanayoendelea Kibiti leo jijini
Dar es Salaam.
Sehemu ya waandishi wa habari
pamoja na Makamanda wa Jeshi la Polisi wakimsikiliza IGP Mpya, Simon
Sirro alipokuwa akizungumza na Wanahabari mapema leo jijini Dar es
Salaam.(PICHA NA JOHN
BUKUKU-FULLSHANGWE-MAMBO YA NDANI)
…………………………………………………………………………..
Mkuu wa Jeshi la polisi Nchini
(IGP),Simon sirro ameahidi kutoa sh.milion 10 kwa yeyote atakayetoa
taarifa za kufanikisha kuwakamata watu wanaofanya mauaji ya viongozi
huko Kibiti wilayani Rufiji Utete mkoani Pwani.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,
Sirro amesema kumekuwa na mauaji ya wananchi na Askari katika Wilaya ya
Rufiji Utete pamoja na Wilaya ya Mkuranga ambayo yamekuwa yakifanywa na
wahalifu wachache kwa malengo wanayoyajua wao,
Amesema Jeshi la Polisi bado linaendelea na Operesheni
mbalimbali kuhakikisha kwamba vitendo hivyo haviendelei kuweza kubaini
mzizi.
Aidha Mkuu wa Jeshi la Polisi Mpya amezungumzia juu ya
waendesha boda boda kuwa na tabia ya kukaidi kufata sheria za usalama
barabarani ikiwemo kubeba abiria zaidi ya mmoja ‘mishikaki.
Sirro amesema waendesha bodaboda wanashindwa kufuata sheria za
usalama barabarani kwa kupita taa nyekundu pamoja na kutovaa kofia ngumu
‘Helment’ ambapo kumesababisha wengine vifo na majeruhi ya kuwafanya
kuwa na ulemavu wa kudumu
Hata hivyo amesema kumekuwa na malalalamiko dhidi ya baadhi ya
Askari polisi kujihusisha na vitendo vya rushwa lakini pia baadhi ya
wananchi kuwashawishi Askari kupokea rushwa ikiwa ni sehemu ya ngao ya
kukwepa kuwajibishwa pindi wanapokuwa wamefanya makosa.
No comments :
Post a Comment