Wednesday, May 10, 2017

KIZAAZAA CHA MVUA ZANZIBAR; SMZ YAFUNGA SHULE ZOTE ZA SERIKALI NA BINAFSI


Mhe.Riziki Juma Pemba
  
NA K-VIS BLOG, ZANZIBAR
KUFUATIA mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kuleta madhara visiwani Zanziban hususan Pemba, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Mhe Riziki Juma Pemba ametangaza rasmi kuzifunga skuli zote za serikali na binafsi kuanzia leo Jumatano Mei 10, 2017 hadi Jumatatu wiki ijayo Mei 15.
Kwa mujibu wa Radio ya Shirika la Utangazaji Zanziba, (ZBC), sababu hasa za kufungwa kwa skuli(shule), kunatokana na kuendelea kunyesha mvua kubwa katika visiwa vya Unguja na Pemba na hivyo kusababisha kujaa maji maeneo mbali mbali na hivyo kuhatarisha usalama wa wanafunzia.
Hata hivyo taarifa hiyo ya serikali imefafanua kuwa wanafunzi wote wanaofanya mtihani ya kidato cha sita, wao wataendelea kwenda shule ili kufanya mitihani yao. Taarifa ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, (TMA), imeonya kuwa leo Mei 10, 2017  hadi Mei 12, 2017, kutakuwepo na vipindi vifupi vya mvua kubwa klwenye ukanda ote wa pwani ya Kaskazini, ikiwemo visiwa vya Unguja na Pemba.
Taarifa kamili yaTMA inaonyesha hapo chini.


No comments :

Post a Comment