Naibu Katibu Mkuu wa CCM
Zanzibar, akiingia ndani ya nyumba ya mkaazi wa shehia ya
miwani Bi. Christina John kumfariji juu ya maafa hayo ya marfuriko ya
mvua visiwani Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM
Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi” akiangalia ukuta
uliobomoka kwa mvua wa vyoo vya Skuli ya msingi na sekondari
Bwejuu na kuchangia sh.200,000 na gari moja la mawe ili ukuta huo ujengwe
haraka ili shule ikifunguliwa wanafunzi wapate huduma ya vyoo.
Bw. Edward Maziku
mmoja kati ya wananchi waliopata maafa hayo ambaye nyumba yake
imepotomoka kutokana na mvua hizo kama inavyoonekana pichani na Dkt.
Mabodi alimpa msaada wa sh.200,000 ili aweze kujikimu huku
CCM na SMZ zikiendelea kutafutia ufumbuzi changamoto ya mafuriko visiwani
Zanzibar
Mwananchi wa shehia ya
Miwani iliyopata athari ya kuharibika kwa miundombinu ya barabara Bw. Mohamed
Sheweji Mohamed ambaye pia ni miongoni mwa waasisi wa ASP akizungumza na
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Saadala “
Mabodi” katika ziara hiyo ya kuwafariji wananchi.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM
Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi” akizungumza na mmoja kati ya
wananchi waliopata maafa ya mvua zinazoendelea kunyesha, Bw. Kassim Vuai
huko Shehia ya Kizimbani Wilaya ya Magharib “ A” Unguja.
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema kinaendekea na juhudi za
kuishauri serikali iharakishe utaratibu wa kutoa misaada kwa wananchi walioathiriwa
na maafa ya mvua ili waweze kupata huduma za msingi kama walivyo wananchi
wengine waliosalimika na tatizo hilo.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Mkuu wa Chama hicho Zanzibar, Dkt.Abdalla Juma Saadala
'' Mabodi" katika mwendelezo wa ziara yake ya kukagua maeneo mbali
mbali nchini yaliyopata maafa ya mvua zinazoendelea kunyesha nchini.
Dkt.Mabodi
aliwambia wananchi hao kwamba serikali ya Mapinduzi ya zanzibar inayotokana na
chama hicho ni sikivu na inathamini maisha na utu wa wananchi wote bila ya
kujali itikadi za kisiasa, hivyo itaendelea kutoa mapendekezo kwa Idara ya
Maafa nchini ifike kila pembe ya visiwa vya zanzibar kuhakikisha wananchi wote
waliopata maafa wanaratibiwa na kupatiwa misaada.
Alieleza
kwamba pamoja na taasisi hiyo kufanya kazi za kisiasa bado ina jukumu la
kuwalinda na kuwasaidia wananchi wakati panapotokea majanga mbali mbali ya
kitaifa ili waweze kubaki salama na kuendelea na shughuli za kimaendeo.
"
Wananchi tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu atuvushe salama katika hii neema ya
mvua iliyochanganyika na mitihani, ili turudi katika maisha ya kawaida na
kuondokana na hofu.
Jukumu
letu kama chama cha kisiasa wakati wa maafa ni kuhakikisha kila mwananchi ana
kuwa salama na kupata huduma za msingi sambamba na kuwafariji huku serikali
ikiendelea kukamilisha taratibu za kutafuta ufumbuzi wa kumaliza
changamoto zinazotokana na maafa hayo." alieleza Dkt. Mabodi wakati
akitoa msaada wa fedha sh.200,000 kwa mwananchi wa Shehia ya Miwani
Unguja, Bw.Endward Maziku ambaye nyumba yake imebomoa na kukosa makaazi
ya kuishi.
Akitoa
ufafanuzi kwa wananchi wa maeneo ya shehia ya Miwani kuwa changamoto ya miundo
mbinu ya barabara inayowakabili , alisema SMZ ina mpango wa
kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwa awamu pamoja na Vijiji vya Koani,
Jendele, Unguja Ukuu na Jumbi.
Alifafanua
kuwa baadhi ya barabara hizo tayari zilikuwa zimeanza kutengenezwa lakini
baadae serikali ikabaini kuwa Mkandarasi aliyepewa tenda hiyo hana sifa
na ikaamua kumfuta.
Sambamba
na hayo Naibu Katibu Mkuu huyo, aliendelea kuwasisitiza waakazi wa maeneo mbali
mbali kutibu maji kabla ya kuyatumia pamoja na kuwa karibu na watoto wadogo
wasicheze karibu na mabwawa ya maji ya mvua kwa lengo la kuepuka athari za
maafa.
"
Nakiri kwamba mvua hizi ni kubwa sana hazijawahi kutokea kwa miaka ya
hivi karibu, kwani mvua kama hizi nakumbuka zilitokea miaka ya 1972-1973 na
kuacha maafa makubwa.
Pia
nawaomba wanasiasa nchini tusitumie maafa haya kama ajenda ya kisiasa bali
tuwafariji na kutoa nasaha za kuwashauri mambo mema na kuwaeleza hali halisi
kwani SMZ na CCM hazipendi wananchi wapate majanga na
migogoro, hivyo mitihani hiyo ni majaaliwa ya Mwenyezi Mungu".alifafanua
Naibu Katibu Mkuu huyo.
Mapema
wananchi hao kwa nyakati tofauti walisifu kasi ya usimamizi wa Ilani ya CCM
inayotekelezwa na Serikali kwa kuimarisha huduma za msingi katika sekta mbali
mbali za kijamii na kiuchumi.
Akizungumza
Mkaazi wa Chwaka Wilaya ya Kati alisema licha ya kuwepo kwa changamoto za maafa
zilizoharibu miundombinu ya maji, barabara na umeme lakini bado wana matumaini
kwa serikali itafanya marekebisho ya haraka kwa baadhi ya huduma ili zilidi
katika hali ya kawaida.
Naye
Mkaazi wa Jambiani Kikadini, Ramadhan Kassim, aliwaomba wananchi wa
maeneo mbali mbali nchini kuwa na utamaduni wa kuwa na tahadhari ya
kujipanga mapema kwa kufuata ujenzi unaozingatia ushauri wa kitaalamu ili
kuepuka maafa wakati wa mvua zijazo.
No comments :
Post a Comment