Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akihitimisha mjadala wa Bajeti ya Wizara
yake ambapo Bunge limepitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya
shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) na Naibu wake Dkt. Ashatu Kijaji
(Mb), wakifuatilia kwa makini hoja mbalimbali za Wabunge wakati
wakijadili Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni Mjini Dodoma, ambapo Bunge hilo
limepitisha Bajeti ya shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa Fedha
2017/2018.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa,
akimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango
(Mb) ndani ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, baada ya wabunge kupitisha
Bajeti ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa,
akimpongeza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji
(Mb) ndani ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, baada ya wabunge kupitisha
Bajeti ya Wizara hiyo ya jumla ya shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa
Fedha 2017/2018.
Mkurudenzi wa Idara ya
Mipango-Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Richard Mkumbo (kulia),
akipongezana na Mkurugenzi wa Bima ya Taifa, kwenye viwanja vya Bunge
Mjini Dodoma baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya wizara hiyo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,
Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akimsikiliza kwa makini Mbunge wa
Babati Vijijini Mhe. Jitu Soni nje ya Ukumi wa Bunge mara baada ya
Wabunge kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo ya shilingi trilioni 11.752 kwa
Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Gavana wa Benki Kuu (BOT), Prof.
Beno Ndullu (kushoto), akimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.
Philip Isdor Mpango (Mb), baada ya Bunge kupitisha makadirio ya Mapato
na Matumizi ya Wizara hiyo ya shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa
Fedha 2017/2018 Mjini Dodoma
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Mpango (Mb) akipeana mkono na Mkaguzi Mkuu wa ndani wa
Serikali Bw. Mohamed Mtonga, nje ya ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma baada
ya Bunge kupitisha bajeti ya Wizara hiyo ya shilingi trilioni 11.752 kwa
Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoro) akimshukuru na kumpongeza Naibu
wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) kwa kazi kubwa aliyoifanya katika
kusimamia na kuhakikisha kuwa Bajeti ya Wizara hiyo inaandaliwa kwa
viwango vya juu na hatimaye kupitishwa na Bunge Mjini Dodoma ambapo
Wizara hiyo imeidhinishiwa kukusanya nakutumia shilingi trilioni 11.752
kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa saba kutoka kushoto mstari wa mbele)
akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakuu wa Wizara na Taasisi
zilizochini ya Wizara hiyo nje ya ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma baada ya
kuhitimishwa kwa mjadala wa bajeti wa Wizara hiyo.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
No comments :
Post a Comment