Bw. Dennis Masami Mkuu wa Kitengo
cha kodi Wizara ya Ardhi akitoa mada kwa wanahabari kwenye semina
kuhusu Kodi za pango ya Ardhi na majengo iliyofanyika wizarani hapo ili
kuwajegea uwezo wanahabari katika masuala ya sheria na taratibu za
ulipaji wa kodi za pango ya Ardhi na kodi za majengo, Semina hiyo ambayo
imeshirikisha pia wataalam wa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA)
imefanyika leo jijini Dar es salaam ikishirikisha waandishi wa habari
kutoka vyombo mbalimbali vya habari pamoja na mitandao ya kijamii.
Baadhi ya wataalamu mbalimbali
kutoka wizara ya ardhi na waandishi wa habri wakiwa katika semina hiyo
iliyofanyika leo wizarani hapo kuhusu masuala ya kodi za pango ya ardhi
na kodi za majengo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika semina hiyo.
Wanahabari wakiandika mambo
muhimu yaliyotolewa katika mada zilizotolewa na wataalam mbalimbali
kutoka wizara ya Ardhi na Mamlaka ya Mapato (TRA) kuhusu Kodi ya Pango
ya Ardhi na kodi ya Majengo.
Maya Magimba Afisa Msaidizi wa Huduma kwa mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA)akitoa mada katika semina hiyo.
Bw. Gabriel Mwangosi Meneja Idara
ya Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi TRA akifafanua jambo wakati akijibu
maswali ya waandishi wa habari kwenye semina hiyo.
Stoney Mkamba Afisa Kodi Mkuu
Makao Makuu TRA akifafanua jambo wakati wa semina hiyo iliyofanyika
kwenye Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi leo jijini Dar es
salaa.
No comments :
Post a Comment