Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akifurahia jambo na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kwenye viwanja
vya Bunge mjini Dodoma Aprili 20, 2017. Wengine kutoka kushoto ni
Wabunge wa Viti Maalum, Cecilia Pareso, Catherene Magige na Joyce
Mukya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mchungaji Dkt. Getrude Rwakatare
akisindikizwa na baadhi ya wabunge kuingia kwenye ukumbi wa bunge mjini
Dodoma ili kuapishwa kuwa mbunge wa Viti Maalum, Aprili 20, 2017.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Spika wa Bunge, Job Ndugai akiongoza kikao cha bunge mjini Dodoma Aprili 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali bungeni mjini Dodoma, Aprili 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kwenye viwanja vya
Bunge mjini Dodoma Aprili 20, 2017. Wengine kutoka kushoto ni Wabunge
wa Viti Maalum, Cecilia Pareso, Catherene Magige na Joyce Mukya. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisikiliza swali wakati alipoulizwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni,
Freeman Mbowe, bungeni mjini Dodoma, Aprili 20, 2017. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisikiliza swali wakati alipoulizwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni,
Freeman Mbowe, (kulia) bungeni mjini Dodoma, Aprili 20, 2017. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye kwenye viwanja vya bunge
mjini Dodoma, Aprili 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………..
- Asisitiza vyombo vya dola vipewe muda wa kufanya uchunguzi wa matukio ya kihalifu
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amewataka Watanzania kuendelea kuiamini Serikali yao na kuvipa muda
vyombo vya dola kuendelea kufanya uchunguzi dhidi ya matukio mbalimbali
ya
kihalifu yaliyotokea nchini ili kubaini chanzo cha matatizo na
wahusika.
Aidha, Waziri Mkuu ametoa wito
kwa Watanzania wote kuendelea na utamaduni wa kushirikiana na vyombo vya
dola kwa kutoa taarifa pindi vinapotokea vitendo vya kihalifu au
viashiria vyake katika maeneo mbalimbali nchini.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo
(Alhamisi, Aprili 20, 2017) Bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha
maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman Mbowe
aliyetaka kupata kauli ya Serikali juu ya hofu iliyotawala nchini kuhusu
vitendo vya watu kuuliwa, kupotea na kutekwa.
Waziri mkuu amesema “tukitoa
taarifa mapema tunaweza kuharibu upelelezi, tuviachie vyombo vetu vya
dola viendelee kufuatilia kuona nani anayesababisha vitendo hivyo na
dosari iko wapi na nini chanzo chake alisisitiza,”.
Kadhalika Waziri Mkuu amewasii
Watanzania kuendeleza utamaduni mzuri wa watu kuheshimiana, kufuata
kanuni na kuviachia vyombo vya dola kutekeleza majukumu yake. “Moja ya
majukumu ya Serikali ni kuhakikisha Watanzania wanaishi kwa amani kwa
kuwa na ulinzi wa uhakika kwao wenyewe na mali zao wakati wote,”.
Hata hivyo, Mheshimiwa Mbowe
aliishauri Serikali kushirikiana na vyombo vya kiuchunguzi vya kimataifa
kuchunguza tukio la kupotea kwa msaidizi wake Ben Saanane lililotokea
miezi sita iliyopita, ambapo Waziri Mkuu amesema kuwa Taifa lina
mahusiano mazuri na mataifa mbalimbali na inashirikiana nayo katika
mambo mbalimbali likiwemo suala ya ulinzi ambapo si rahisi kuainisha
namna wanavyoshirikiana.
Waziri Mkuu ameongeza kuwa vyombo
vyetu vina weledi,vifaa na uwezo wa kutosha kufanya uchunguzi juu
mambo yanayotokea nchini hivyo amesisitiza wananchi kuendelea kuiamini
kwani matukio haya ya kihalifu likiwemo la mtu kutoweka au kufariki na
haina kikomo cha uchunguzi, mara zote uchunguzi unategemeana na aina ya
tukio lenyewe au mazingira lilipo tokea
Katika hatua nyingine, Waziri
Mkuu amesema Serikali inafanya mapitio kwa vyama vyote vya Ushirika
nchini kufuatia baadhi ya vyama hivyo kuwa na mwenendo mbaya hali
inayochangia upotevu wa fedha nyingi na kukatisha tamaa wakulima.
Amesema hivi karibuni katika
kikao cha wadau wa zao la korosho kilichofanyika wilayani Bagamoyo Bodi
ya Korosho ilidaiwa kuhusika na ubadhilifu wa sh. bilioni 30 ambapo
Serikali iliunda timu maalumu ya uchunguzi na kubaini upotevu wa sh.
bilioni sita na siyo sh. bilioni 30.
Hata hivyo amesema kwamba hasara
hiyo ya sh. bilioni sita haikusababishwa na bodi bali vyama vikuu na vya
ushirikika vilivyopo kwenye ngazi ya Kata na wilaya, ambavyo vyote
vilifanyiwa uchuguzi na hatua zimeanza kuchukuliwa.
Amesema matatizo hayo yako katika
vyama vyote vya ushirika hususan vya mazao ya Tumbaku, Kahawa,Pamba,
Chai na mazao mengine makuu, ambapo Serikali imeanza kupitia taarifa za
ukaguzi kwa kina ili iweze kufanya ukaguzi na sasa wanaendelea na
uchunguzi wa chama kikuu cha tumbaku.
Waziri Mkuu amesema wakimaliza
kufanya uchunguzi katika chama kikuu cha tumbaku watachunguza vyama
vingine vya pamba, kahawa na chai lengo likiwa ni kuwalinda wakulima na
kuhakikisha wanapata tija. “Naomba kusisitiza hatua zinaendelea
kuchukuliwa na tutaendelea kuimarlisha na ushirika,”.
Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati
akijibu swali la Mheshimiwa Mama Salma Kikwete aliyetaka kujua hatua
zilizochukuliwa na Serikali kuhusu ubadhirifu wa sh. bilioni 30
uliofanywa na Bodi ya Korosho nchini.
No comments :
Post a Comment