NA
JUDITH MHINA - MAELEZO
Waziri
Mkuu mstaafu wa Awamu ya Kwanza Dkt Salim Ahmed Salim amesema ili muungano wa Tanganyika na Zanzibar
uweze kudumu na kuimarika hatuna budi kuelezea mafanikio yalitopatikana na pia kutafuta
ufumbuzi wa ...
kero chache zilizopo.
kero chache zilizopo.
Dkt,
Salim Ahmed Salim amesema hayo leo jijini Dar Es salaam wakati wa mahojiano na Idara
ya Habari – MAELEZO kuhusiana namaadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika hizi karibuni.
Warizi
huyo msataafu amekiri kwamba Watanzania wana haki ya kujivunia muungano huu
ambao ni wa asili kutokana na mahusiano yetu ya kindugu hata kabla ya Muungano. “Mahusiano ya kindugu baina ya Wananchi wa
Tanganyika na Zanzibar ni ya miaka mingi ambapo watu wake wamekuwa
wakitembeleana na kuoana. Aidha, mahusiano hayo yameonekana katika masualoa ya
kijamii kama vile lugha, dini n.k.
Dkt
Salim ameeleza kwamba, walichokifanya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere na Hayati Shekh Abeid Amani Karume ni kuweka uwazi juu ya
mahusiano ya watu wa Tanganyika na Zanzibar duniani hususan kwa wale ambao
hawajui asili ya watu wa pande hizo mbili.
“
Jambo hili la Muungano kudumu miaka 53 linashangaza watu wengi duniani, hasa kwa
dhana kwamba nchi za kiafrika zina matatizo, na sio rahisi kuelewana. Jambo kubwa linalofanikisha kudumu kwa Muungano wetu ni umoja, upendo na mshikamano.
Tumekuwa tukuweka wazi mafanikio na pale penye changamoto hukaa pamoja na kuzungumza
ili kuyapatia ufumbuzi.”
Akizungumzia
suala la vijana kushika madaraka Serikalini, Dkt Salim amesema “Hii si jambo
geni kwani mimi ndiye kijana wa kwanza ambaye
niliaminika nikiwa mdogo sana miaka 22 na kuteuliwa kuwa Balozi nchini Misri.
Kazi hii haikuwa ndogo lakini niliifanya kazi kwa kujiamini na kwa uadilifu
mkubwa huku nikipata maelekezo kutoka kwa viongozi wangu wakuu (Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar).
Hivyo
napenda kuchukua nafasi hii kutoa wito kwa Watanzania wenzangu hususan vijana wanaoaminiwa
na Taifa katika umri mdogo kushika uongozi wakubali nafasi hizo kwa kuwa bado
wana nguvu ya kuweza kulitumikia Taifa letu. Lakini wasisahau kuwasikiliza viongozi
waliowapa nafasi hizo, na ushauri wa wazee ni muhimu sana. Aidha, wajue kuwa nafasi
za uongozi wanazomepewa kuwawakilisha Watanzania zilete maendeleo ya kweli.
Akielezea
mustakabali wa maendeleo ya nchi, Dkt Salim alitolea mfano wa vijana wa Afrika
ya Kusini ambapo hivi katibu alikwenda kushiki moja ya mikutano viongozi wa
nchi za Afrika. hivi Amesema, vijana wa Afrika ya Kusini hawataki kusikia
lolote zaidi ya mambo yanayowahusu wao na maisha yao. Hawajui kama kuna watu
wamepigania uhuru na hatimaye ukombozi wa nchi yao. Wao hilo si kipaumbele kwao, wanachotaka
ni maendeleo ambayo yatagusa maisha yao.
“Hivyo
ni vema Serikali zetu zilivyoamua kuelekeza nguvu katika viwanda vidogo vya
kati na vikubwa, kwa sababu malighafi tunazo za kutosha ila tulikosa mbinu za
kuongeza thamani ya malighafi zetu. “Nataka nikuhakikishie tuko kwenye njia
sahihi ili kuwafanya vijana walio wengi washiriki katika kulijenga Taifa na
kupata ajira ambazo zitawafanya waishi kwa furaha na matumaini,” Asema Dkt
Salim.
Akijibu
swali, kuhusiana na lipi la kujivunia kutokana na Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar Dkt Salim amesema : “ Umoja wetu ndio uliotufikisha miaka 53,
tusingekuwa wamoja tungegawanyika na Muungano ungekuwa mashakani. Angalia idadi kubwa ya Watanzania sasa ni
wale waliozaliwa baada ya Muungano ambao hawajui lolote kuhusu Muungano.
Tuna
Jukumu kubwa la kuendeleza elimu ya historia kwa vizazi vya sasa na vijavyo
waelewe na kudhamini kazi zilizofanywa na waasisi wetu wa Muungano Mwalimu
Nyerere na Shekh Karume. Mfano mzuri ni Taifa la China ambalo vijana wengi hawakuwahi
kumuona Mao SeThung, lakini wanamjua kutokana na historia wanayoelezwa na
matunda yake ambayo wanayaona.
Pili,
Watanzania tusibaguane kama alivyosema Mwalimu Nyerere kwamba dhambi ya ubaguzi
haiwezi kuishia hapo unapombagua mtu, itaendelea kwa mwingine na mwingine na mwisho
Taifa litagawanyika.
Aidha,
Dkt Salim amesema kwamba Taasisi ya Mwalimu Nyerere itaendelea kutoa elimu ya
umuhimu wa muungano ambao ni tunda la umoja na mshikamano barani Afrika,
hususani Tanzania ambao wanahitaji kuwa na elimu ya uraia.
Mwisho
alimalizia kwa kutoa wito kwa Watanzania kuuenzi na kudumisha muungano wetu
ulioanzishwa na Waasisi wetu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Shekh Abeid
Amani Karume.
SKIMU 7 ZA UMWAGILIAJI WILAYANI MBARALI ZATOZWA FAINI KWA KUTOZINGATIA SHERIA YA MAZINGIRA
Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa Kikosi kazi cha kitaifa cha kutathmini Ikolojia ya Mto Ruaha Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya. |
Kikosi kazi cha kitaifa cha kutathmini Ikolojia ya Mto Ruaha kikiwa katika moja ya skimu za umwagiliaji Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya |
No comments :
Post a Comment