Friday, April 28, 2017

RAIS MAGUFULI ACHARUKA, AAGIZA WATUMISHI WA UMMA 9,932 WALIOGUSHI VYETI WAKATWE MSHAHARA WA APRILI NA KUFUTWA KAZI

NA K-VIS BLOG
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amepokea taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma kwenye ukumbi wa Chimwaga, chuo kikuu cha Dodoma UDOM leo Ijumaa Aprili 28, 2017.
Profesa Ndalichako
Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Rais Magugfuli amesema, watumishi wote wa umma 9,932 waliobainika kuwa na vyeti vya kugushi, wakatwe mshahara wa mwezi huu wa wa nne na waondolewe kwenye utumishi wa umma kuanzia leo Aprili 28, 2017.
Akifafanua zaidi, alisema watumishi hao wajiondoe wenyewe kabla Mei 15 vinginevyo wafikishwe mahakamani.
Awali akitoa taarifa ya zoezi hilo la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako, alisema,  taarifa aliyokabidhiwa Mhe. Rais, ni  ya awamu ya kwanza iliyohusisha watumishi wa serikali za mitaa, taasisi, mashirika ya uma na wakala wa serikali, taarifa ya watumishi wa serikali kuu itawasilishwa katika awamu ya pili
“Wizara yangu ndiyo yenye jukumu la kutunuku vyeti katika kada mbalimbali. Tulianzisha uatratibu wa kuweka picha kwenye vyeti, lakini pia tumeunganisha mifumo ya udahili ya mafunzo ya elimu ya kati na ya juu kwenye kanzi data ya mitihani.”
Mhe. Angella Kairuki
Tumeweka alama ficho ili kuwabaini wale wanaogushi vyeti, lakini tuliagiza waajiri kuhakikisha wanapatiwa vyeti ili kuhakiki wale wanaowaajiri, jumla ya vyeti 137,504 viliwasilishwa, vyeti 9,932 sawa na asilimia 3.8% vilikuwa vyeti vya kugushi.
“Leo tunaandika historia ya kipekee katika historia ya nchi hii kwani zoezi hili ndio limefanyika kwa mara ya kwanza tangu nchi hii ipate uhuru, tunakupongeza kwa kusimamia ipasavyo kile unachozungumza.” Prof. Ndalichako
“Tumehakiki vyeti vya kidato cha nne, cha sita, ngazi ya cheti cha ualimu. Bado ngoma mbichi bado hatujaanza kuhakiki vyeti vya kitaaluma”.
“Waliojiunga na elimu ya chuo kikuu kwa vyeti vya kugushi wajisalimishe kwani njia za mkato zimefungwa”
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (Utumishi na Utawala bora), Mhe. Angella Kairuki, Wizara hii uliyonipa dhamana ya kuisimamia, inalo jukumu la kusimamia sheria, na kanuni ili kutekeleza utawala bora. Serikali haiwezi kufikia azama yake ya kujenga uchumi wa viwanda kama serikali itaajiri wataalamu wenye utaalamu wa bandia, kwani patakiwa na watumishi wasio na uwezo stahili.
Ofisi yangu kwa kushirikiana na wizara ya elimu, sayansi na teknolojia, tulianzisha zoezi la kuhakiki vyeti vya kidato cha nne, sita na vyeti vya ualimu ili kubaini wale wote wenye vyeti visivyostahili.
“Zoezi hili halikuhusisha watumishi wa kisiasa kama vile mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya na madiwani. Hii ni kwa mujibu wa ibara ya 67 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”., Kairuki.
Waziri Kairuki alisema tayari watumishi 435,000 wamehakikiwa,  Asilimia 94.23 ya waliohakikiwa wana vyeti halali, aidha watumishi 9,932, wamebainika kuwa na vyeti vya kugushi.
Kundi la tatu ni lile lenye watu wenye vyeti vyenye utata, ilibainika kuwepo kwa watumishi wenye chiti kimoja kutumiwa na zaidi ya mtu mmoja ni 1,538.
Rais Magufuli, na Prof.Kikula wa UDOM
Kundi la nne ni la watumishi waliowasilisha vyeti pungufu ni 11, 596, waliwasilisha vyeti vya utaalamu pekee lakini hawawasilisha vyeti vya kidato cha nne na sita.
Naye Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alisema ”Eimu ni hatua na kujifunza nako ni mchakato, kwa hiyo wale wote ambao wameonekana hawakuwa na vyeti ambavyo sio halali, basi tunaweza ksuema wka wale waliofikia ukomo kwa maana ya kupata daraja la chini anatakiwa kufanya mtihani binafsi ili kufikia daraja hilo, lakini kwa wale wote ambao wameharakisha na ambao wametamkwa kwenye taarifa hii na ambao ni watumishi, wajue wametenda kosa, na hivyo mhe. Rais watu hao wamepoteza sifa za utumishi wa umma.” Alisema Mhe. Majaliwa.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti kwa Watumishi wa umma kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki katika Ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe katika vitabu hivyo vya taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma alivyopokea kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki katika Ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma. Katikati ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na wakwanza kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Profesa Idris Kikula.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa kitabu cha Taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma alivyopokea kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki katika Ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma. Katikati ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na wakwanza kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Profesa Idris Kikula.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinyanyua juu Taarifa na vitabu vye majina 9,932 ya watumishi wenye vyeti vya kugushi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe na kufungua boksi kubwa lenye majina ya watumishi zaidi ya 9,932 waliobainika kuwa na vyeti vya kugushi mara baada ya kupokea Taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki katika Ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia majina hayo pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kufungua boksi kubwa lenye majina ya watumishi hao wa umma ambao wamegushi vyeti vyao .
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisoma jina mojawapo la mtumishi aliyegushi cheti katika taarifa hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakiangalia vitabu vyenye majina ya watumishi wa Umma zaidi ya 9,932 waliogushi vyeti vyao vya elimu ya Sekondari.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa , Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako, Spika wa Bunge Job Ndugai, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki wakiminya kitufe kuashiria maadhimisho ya miaka 10 ya Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM katika ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma.

No comments :

Post a Comment