Thursday, April 20, 2017

WACHUNGAJI ZAIDI YA 300 WA MADHEHEBU MBALIMBALI KUSHIRIKI SEMINA NA KONGAMANO JIJINI ARUSHA

SAM_0052
Mch.Dr.Jerry Williamson
kutoka nchi  Marekani akiomba katika ibada ya  katika kongamano kanisa la
Zion lililopo njiro jijini Arusha ambapo kanisa hilo limeendaa semina na
kongamano  kwa wachungaji pamoja na washirika wengine,kulia kwake ni
Ben Mangeni ambaye ni mkalimani wake

 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kongamano hilo
Mch.George Mngodo akiongea na waandishi wa habari , alisema kuwa watu ambao wataweza kushiriki kongamano hilo wataweza kujifunza
mambo ambayo awali hawakuweza kuyafahamu ambayo yatawawezesha  kuvuka kutoka hatua moja kwenda nyingine
Mmoja wa wachungaji wa
kanisa hilo Paul Sulley akiongea na waandishi wa habari alisema kuwa matarajio yao ni kuona kila mtumishi
anayehudhuria anavuviwa upya ili aweze kumtumikia Mungu kwa  bidii.
 kushoto ni Mtume trice Shumbusho akiwa na mkalimani wake akihubiri katika kongamano  hilo
Waumini wakiwa katika maombi
Baadhi ya wageni wakiwa katika kanisa la Zion kwaajili ya kongamano
 
 Baadhi ya wageni wakiwa katika kanisa la Zion kwaajili ya kongamano
Picha ikionyesha madhabahuni
 Picha ikionyesha jengo la kanisa

Na Pamela Mollel,Arusha
 
Wachungaji zaidi ya 300
kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini bila kujali madhehebu yao  wako katika semina maalumu ya neno la Mungu yenye
lengo la kusaidia kupeleka ujumbe wa madhihilisho ya nguvu ya kristo katika maeneo
mbalimbali ya nchi ili watu waweze kubadilika na kumjua Mungu
 
Semina hiyo ya siku
nane iliyoandaliwa na kanisa la Zion City Church Arusha   litafanyika
kanisani hapo   ikiambatana na Kongamano  ambalo limeandaliwa kwa ajili ya wachungaji na
watu mbalimbali likiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa kupeleka injili kwa watu
wa mataifa.
 
Mwenyekiti wa kamati ya
maandalizi ya kongamano hilo Mch.George Mngodo alisema kuwa watu ambao wataweza
kushiriki wataweza kujifunza mambo ambayo awali hawakuweza kuyafahamu ambayo
yatawawezesha  kuvuka kutoka hatua moja
kwenda nyingine.
 
 Mngodo aliongeza kuwa  huduma zitakazo tolewa katika katika
kongamano hilo hazitawakugusa kiroho tu bali hata kwenye maisha yao ya kawaida
wataweza kubadilika
 
“Tunaamini kongamnao
hili litagusa wachungaji hawa na jamii wanayoihudumia kimwili na kiroho”alisema
Mngodo
 
Kwa upande wake mmoja
wa wachungaji wa kanisa hilo Paul Sulley alisema kuwa matarajio yao ni kuona
kila mtumishi anayehudhuria anavuviwa upya ili aweze kumtumikia Mungu kwa  bidii.
 
Mch.Sule alisema kuwa ulimwengu
wa sasa umeharibika hivyo unahitaji watumishi waliokutana na Mungu na si
wanaomjua Mungu pekee ili waweze kuwatumikia watu.
 
Miongoni mwa watumishi
wa Mungu wa kimataifa watakao kuwa wasemaji wakuu katika kongamano hilo ni Askofu
mkuu wa kanisa la Zion City Church Arusha   John
Shumbusho pamoja na mkewe Trice Shumbusho
  Wachungaji
 wengine ni kutoka nje ya nchi Mch.Dr.Jerry
Williamson, Mch.Dr Jim Oxendine kutoka Marekani,Mch.Yoshua Masasu kutoka
Rwanda,Mch.Aloysius Kiiza kutoka Uganda,Pamoja na Mch.George Mkandawire kutoka Afrika
Kusini  .

No comments :

Post a Comment