Thursday, April 20, 2017

UTEUZI WA MWENYEKITI NA WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI YA WAKALA WA NISHATI VIJIJINI (REA)

PROF MUHONGO

Mhe. Prof. Sospeter M. Muhongo (Mb.), Waziri wa Nishati na Madini, ameteua Mwenyekiti na Wajumbe Wapya wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kutokana na Mamlaka aliyonayo chini ya Kifungu Nambari 5(1) (b) na Nambari 8(3) cha Sheria ya Nishati Vijijini ya mwaka 2005.

Wajumbe wapya walioteuliwa kwa kipindi hicho ni:
  1. Gideon Kaunda –  Mwenyekiti
  2. Innocent G. Luoga –  Mjumbe
  3. Happiness Mhina –  Mjumbe
  4. Stella Mandago –  Mjumbe
  5. Scholastica H. Jullu – Mjumbe
  6. Amina H. Chinja –  Mjumbe
  7. Theobald Sabi        –  Mjumbe
  8. Michael P. Nyagoga –  Mjumbe
Uteuzi huo ni wa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia tarehe 1 Aprili, 2017.


Imetolewa na Prof. James Mdoe
Kaimu Katibu Mkuu
Aprili 20, 2017

No comments :

Post a Comment