Mwanasheria; Rachel Kilasi –
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , akifafanua sheria ya
Ardhi na. 4 ya mwaka 1999 sambamba na Umiliki wa Ardhi (Haki, Wajibu na
uzingatiaji wa ulipaji wa Pango la Kodi ya Ardhi kwa Mmiliki).
………………..
Mwananchi yoyote ana haki ya
kupatiwa Hatimiliki ambayo ni nyaraka halali ya umiliki wa ardhi baada
ya kupata ridhaa ya Kamishna au Kamati na kulipa ada stahili. Hatimiliki...
hutolewa ndani ya siku 90 mpaka 180 baada ya ridhaa husika.
Katika fungu la 32 la Sheria ya
Ardhi ya namba 4 ya mwaka 1999, masharti ya umiliki wa ardhi
yanaainishwa kuwa ni ya aina tatu, ambayo ni; Umiliki wa miaka 33,
umiliki wa miaka 66 na umiliki ulio mkubwa zaidi ni wa miaka 99.
Aidha, katika fungu la 33 la
Sheria ya Ardhi ya namba 4 ya mwaka 1999, inaeleza sharti la mmiliki wa
ardhi katika kutoa malipo ya pango la Ardhi kwa kila mwaka wa fedha
unapoanza.
Mwananchi hana budi kutimiza
masharti ya ulipaji kodi ya pango la Ardhi kwa wakati. Mwananchi
anapokiuka sharti hili; fungu la 49 – 50 la Sheria ya Ardhi ya namba 4
ya mwaka 1999 inaeleza gharama zake ni pamoja na kutozwa tozo au riba,
Kupelekwa Mahakamani na Kufutiwa umiliki wa ardhi.
Mwananchi zingatia ulipaji wa Kodi la Pango la Ardhi, kutimiza wajibu wako, kuondoa usumbufu na kuongeza pato la Taifa Letu.
Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
No comments :
Post a Comment