Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
akichangia hoja wakati wa kujadili makadirio ya Bajeti ya Ofisi yake kwa
mwaka 2017/2018 Bungeni Dodoma Aprili 11, 2017, aliyekaa ni Naibu wake
(Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipongezana na baadhi ya Watendaji wa Ofisi yake mara baada ya
Kupitishwa kwa makadirio ya Bajeti ya ofisi yake kwa mwaka 2017/2018
Dodoma Aprili 11, 2017.
Ni baadhi ya Watendaji wa Ofisi
ya Waziri Mkuu wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya Bajeti yao
kupitishwa Bungeni Dodoma Aprili 11, 2017 katikati ni Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama na wakwanza kulia ni Naibu wake Mhe. Antony Mavunde.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Ofisi yake Nje ya
Ukumbi wa Bunge mara baada ya kupitishwa kwa Makadirio ya Bajeti ya
Ofisi yake kwa mwaka 2017/2018 Dodoma, kushoto kwake ni Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama.
(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU -DODOMA).
………………
Na. Mwandishi Wetu
Serikali imedhamiria kujenga
Kituo cha Kitaifa cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura
kitakachosaidia katika kukabiliana, kuzuia na ...
kurejesha hali pindi
maafa yanapotokea.
Hatua hiyo ya Serikali ya kuanza
kujenga kituo hicho katika eneo la Miuji mjini Dodoma inakuja huku
idadi kubwa ya wakazi ikiwa inaongezeka kutokana na Wizara na baadhi ya
Taasisi zake kuhamia huko.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista
Mhagama alipokuwa akijibu hoja za wabunge wakati wa kupitisha Makaridio
na matumizi ya bajeti ya ofisi yake kwa mwaka 2017/2018 mapema mwisho
mwa wiki hii Bungeni Dodoma.
“Kwa kutambua umuhimu wa kuwa na
kituo hicho cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura, Serikali
inaamini pindi kitakapokamilika kitakuwa na msaada mkubwa kitaifa
katika kuokoa maisha ya watu na mali zao’’ alisisitiza Mhagama.
Pamoja na hilo waziri alieleza
tayari wadau mbalimbali wameanza kujitokeza na kuunga mkono hatua hizo
ikiwemo Ubalozi wa Israel walipofanya ziara kujionea eneo husika na
kuonesha nia ya kuunga mkono jitihada hizo.
“Tayari Washirika wa Maendeleo
wameshajitoa na kuonesha nia ya kusaidia ambapo walikuja na kuongea na
Ofisi ya Waziri Mkuu na kutembelea eneo hilo.”Alisema waziri Mhagama.
Aidha Ofisi ya Waziri Mkuu imeshatenga fedha na kubaini mipango ya kusaidia kutekeleza ujenzi wa kituo hicho.
No comments :
Post a Comment