Thursday, April 13, 2017

SAKATA LA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI LACHUKUWA SURA MPYA KONDOA


images
Na Mahmoud Ahmad Kondoa
Sakata la wachimbaji wadogo wa madini na Kampuni ya Kidee Minningi limechukuwa sura mpya baada ya Mwenyekiti wa kijiji cha Changaa Kenyata Athman Kukiri  kampuni hiyo kukiuka makubaliano ya mkutano mkuu wa wananchi wa kijiji hicho.
Akizungumza baada ya uongozi wa kumucha kufika ofisini kwake kwenda kuomba PML za
kikundi zilizohifadhiwa ofisini hapo mwenyekiti huyo alisema kuwa ni kweli makubaliano yao ya kukisaidia kikundi hicho ili kiweze kupata leseni yamekiukwa na kampuni hiyo kwa kutangulia kuja na leseni kabla ya mkutano mkuu haujakaa.
Athman alisema kuwa kwenye mkutano mkuu wa kijiji na mwekezaji huyo  atakisaidia kikundi hicho kupata leseni jambo ambalo hajalitekeleza hadi leo tunavyoongea pia aliahidi kukisaidia kikundi kuwepo kisheria nay eye ndio amekuwa wa mwanzo kutonyesha ushirikiano alioahidi mbele ya mkutano wa wananchi.
“Suala hili ni kweli nilifikisha katika mkutano mkuu wa kijiji ili muwekezaji apate Baraka za kupata muhtasari lakini kikundi cha KUMUCHA kilihoji uhalali wa muwekezaji kuanza kazi eneo ambalo vijana walishaanza kazi za uchimbaji mdogo na ndipo alipoandikia ofisi ya kijiji barua ya kulalamika kuvamiwa na mwekezaji,na ndipo mwekezaji akiwakilishwa na meneja wake Ismail Kidee alisema anakitambua kikundi na watashirikiana nao jambo ambalo halikutimizwa na kampuni hiyo”alisema Athman.
Hata hivyo wanakikundi hawakuridhishwa na majibu hayo ndipo wakatoa katiba yao isomwe hadharani ili wananchi watambue haki zao za msingi jambo ambalo meneja wa kidee alikiri kuwa hiki ni kikundi kinachostahili kushirikiana nacho jambo lilipingwa vikali na KUMUCHA kwa misingi nao waliwasilisha mbele ya mkutano huo maopmbi ya muhtasari wa kuomba leseni.
Baada ya mkutano huo matarajio ya kikundi hicho ni kupewa muhtasari lakini kutokana na kauli ya mwekezaji kwenye ofisi ya kijiji ni kuwa yeye ni mwenye dhamana ya kikundi na siyo wao kupewa leseni bila kujali wao ndio waanzilishi wa shughuli za uchimbaji kupitia PML walizopewa na wizara ya madini.
Akizungumza mara baada ya kufika ofisi ya kijiji cha Changaa Mwenyekiti wa kikundi cha KUMUCHA  Donmilaan Shirima alisema kuwa baada ya mwekezaji kufikisha vitendeakazi vyake eneo husika walitumia migambo wa kijiji kuwa ndio walinzi wa eneo la mgodi kupitia serikali ya kijiji jambo ambalo lilitufanya kuiandikia barua serikali ya kijiji bkutoa taarifa za uvamizi wa mwekezaji huyo.
Amesema kuwa cha kushangaza hatua ya barua yetu haikufanyiwakazi na badala yake muhtasari alipewa muwekezaji na sisi kuachwa kuwa ni watumwa kwenye eneo letu,sisi tukabakia na mashangao wa kutoheshimiwa kwa kikundi ambacho kinatambuliwa kisheria.
“Unajua suala hili limekuwa likitushangaza kwa mamlaka za serikali kutoa  eneo mmoja kwa watu wawili ambapo kikundi kilipewa PML halafu anakuja mwekezaji na leseni kwenye eneo hilo kabla ya mkutano mkuu kumpa ridhaa ya umiliki wa eneo jambo linalotia shaka utendeji wa mamlaka za serikali za vijiji na wizara husika”alisema shirima
Hata hivyo ofisa wa madini mkoa wa Dodoma (RMO)hadi sasa haijatuita kwenye mazungumzo ambayo kamishna msaidizi wa madini kanda ya kati alituahidi kushirikishwa kwenye kikao cha mwekezaji na kampuni ya milenium builders japo kikao hicho kimeshafanyika kwa awamu ya kwanza bila kumucha kushirikishwa

No comments :

Post a Comment