Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya
Takwimu Bi. Albina Chuwa akitoa maelekezo wakati alipotembelea kukagua
maendeleo ya ujenzi wa Jengo jipya la Makao Makuu ya Ofisi hiyo
unaondelea Mkoani Dodoma leo (jana), wa kwanza kulia ni Injinia Lan
Shuiqing kutoka Kampuni ya Hainan Internationa.
Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya
Takwimu Bi. Albina Chuwa akitoa maelekezo wakati alipotembelea kukagua
maendeleo ya ujenzi wa Jengo jipya la Makao Makuu ya Ofisi hiyo
unaondelea Mkoani Dodoma leo (jana).
Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya
Takwimu Bi. Albina Chuwa akitoa maelekezo wakati alipotembelea kukagua
maendeleo ya ujenzi wa Jengo jipya la Makao Makuu ya Ofisi hiyo
unaondelea Mkoani Dodoma leo (jana), wa kulia ni Mkurugenzi wa Kampunu
ya Anova Consult Injinia Kitery Kamaley.
Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya
Taifa ya Takwimu Bi. Albina Chuwa akitoa maelekezo wakati alipotembelea
kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo jipya la Makao Makuu ya Ofisi hiyo
unaondelea Mkoani Dodoma leo (jana),katikati ni Mkurugenzi wa Kampunu ya
Anova Consult Injinia Kitery Kamaley.
Msimamizi Mkuu kutoka Kampuni ya Y
and P Bw. Mtumwa Somvi wa kwanza kulia akitoa maelezo kutoka kwa
Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Albina Chuwa wakati
menejimenti ya Taasisi hiyo ilipokagua maendeleo ya
ujenzi mkoani Dodoma leo (jana).
Baadhi ya mafundi wakiendelea na
ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu lenye urefu
wa ghorofa tano linaloendelea kujengwa Mkoani Dodoma.
Muonekano wa ujenzi wa jengo la
Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu unavyoendelea mkoani
Dodoma.(Picha na Benjamin Sawe -Maelezo).
………………..
Benjamin Sawe
Maelezo
Dodoma
MKURUGENZI Mkuu wa Ofisi ya Taifa
ya Takwimu (NBS) Dk. Albina Chuwa ametaka ujenzi wa makao makuu ya ofisi
hiyo unaoendelea mjini Dodom ukamilishwe kwa wakati.
Akizungumza mjini hapa jana baada
ya kukagua ujenzi wa ofisi hiyo, Dk. Chuwa alisema ni wakati sasa kwa
NBS kuwa na ofisi yenye hadhi kwa ajili ya kuboresha na kuimarisha
shughuli
za takwimu nchini.Dk. Chuwa alisema NBS ni miongoni mwa taasisi kongwe nchini na ambayo imekuwa ikibadilika na kwenda na wakati hivyo kupatikana kwa jengo hilo ni jambo linalopaswa kutimia haraka.
“Jengo letu ni la ghorofa tano tu, kwa kuwa mkandarasi umepewa muda wa miezi 10 sioni sababu ya kuchelewa kukamilishwa.
“Hivi karibuni nilizungumza na
wenzetu wa Uganda wao walijenga jengo lao la ghorofa 12 kwa mwaka mmoja
tu sasa sioni sababu kwa nini letu lisikamilike kwa wakati,”alisema.
Kwa mujibu wa Dk. Chuwa jengo hilo
litakuwa ni la ghorofa tano na kwamba kwa kuwa wanazo ofisi katika kila
mkoa nchini, makao makuu hayo yatatumika kuratibu uendeshaji wa
shughuli za takwimu na mambo mengine ya maendeleo yanayohusiana na NBS.
Dk. Chuwa alisema jengo hilo
litagharimu sh. Bilioni 11.6 hadi kukamilika kwake fedha ambazo
zinatokana na mkopo kutoka Benki ya Dunia.
Kwa upande wake, Msimamizi Mkuu wa
ujenzi huo, Mtumwa Shomvi kutoka kampuni ya Y&P Achtects Limited,
alisema watahakikisha wanatekeleza majukumu yao kikamilifu katika
kuusimamia mradi huo.
Shomvi alisema jukumu kubwa wanalolisimamia ni kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati, gharama na ubora uliokubaliwa.
Shomvi alisema jukumu kubwa wanalolisimamia ni kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati, gharama na ubora uliokubaliwa.
Aidha, Msimamizi kutoka kampuni
inayotekeleza mradi huo ya Hainani International Limited ya China, Lan
Shuiqing alisema kazi ya ujenzi inaendelea vyema na kwamba anaamini kila
kitu kitakamilika kwa wakati.
No comments :
Post a Comment