Bidhaa zinazotumika umeme wa jua zinazosambazwa na Mobisol Tanzania
Wafanyakazi wa Mobisol wakionyesha baadhi yabidhaa za kampuni katika promosheni iliyofanyika hivi karibuni
Chaji za sola za Mobisol
…………..
Kampuni ya Kijerumani ya Mobisol inayosambaza nishati ya umeme wa jua na vifaa imara na vya kisasa vinavyotumia nishati hiyo nchini imezindua kampeni maalumu ya kuhamasisha wananchi kujiunga na mtandao wake inayojulikana kama “Hamasika na Masika”.
Kupitia
kampeni hii wateja watakaonunua mitambo ya umeme wa nishati ya jua
katika kipindi cha mwezi huu mwa Aprili na Mei wataingia kwenye droo na
kuweza kujishindia pikipiki aina ya Boxer na pia zaidi ya shilingi
milioni 4 zimetengwa wa ajili ya kutoa zawadi za fedha taslimu kwa
washindi ambapo pia wateja wa sasa wa Mobisol watakaoshawishi wateja wapya kujiunga na mtandao wa Mobisol nao watashirikishwa na droo ya kwanza itafanyika wiki hii.
Meneja Chapa wa Mobisol Tanzania, Seth Mathemu anasema “Tunataka
wateja wetu waweze kunufaika zaidi katika kipindi hiki kwa kuweza
kujishindia zawadi mbalimbali pale wanaponunua mtambo wao wa Mobisol. Ni
utamaduni wetu kugawana sehemu ya faida yetu na wateja wanaoifanya
Mobisol kuwa kampuni bora ya sola katika ukanda wa Afrika mashariki”
Matheme
alisema Shindano hili linawajumuisha wakazi wote wa mikoa zaidi ya
ishirini Tanzania bara ambapo Mobisol inatoa huduma zake na kuitaja
mikoa hiyo kuwa ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Singida, Dodoma,
Tabora, Shinyanga, Mwanza, Mara, Kagera, Simiyu, Geita, Kigoma, Rukwa,
Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe, Pwani pamoja na Morogoro.
Aliongeza kusema kuwa kampuni ya Mobisol inauza na kufunga, mitambo ya bora ya Sola nchini pamoja na vifaa vya matumizi ya nishati hii ambavyo ni Paneli
ya Sola, betri, taa, Televisheni, Radio, Tochi, Mashine ya Kunyolea
nywele, MobiCharger (Kifaa cha kuchajia Simu) na Friji.
“Wakati
ni huu kwa watanzania kupata nishati bora ya umeme wa jua na vifaa vya
kisasa na natoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa hii kujiunga na familia ya Mobisol waweze kuishi maisha ya kisasa na
kujishindia zawadi kupitia kampeni hii ya ‘Hamasika na Masika’.Kwa
maelezo zaidi ya kupata huduma za Mobisol mteja anaweza kupiga simu
namba 0800 755 000 bure na utahudumiwa.Alisema
No comments :
Post a Comment