Timu ya kandanda ya AC Milan ya
Italia imeuziwa kampuni moja ya Uchina na kutia kikomo umiliki wake na
aliyekuwa wakati mmoja Waziri Mkuu wa nchi hiyo na tajiri Silvio
Berlusconi.
Kampuni ya China Rossoneri Sport
Investment Lux, imekamilisha mkataba wa kuinunua timu
hiyo kwa kima cha
dola milioni 628, huku ikiwa na matumaini ya “kuongeza faida mara dufu”.
Klabu hiyo ya Serie A imekuwa chini ya umiliki wa bilionea Silvio Berlusconi, tangu mwaka 1986.
Katika kipindi hicho chote, AC
Milan ilifaulu kunyakua mataji manane katika ligi kuu na kunyakuwa kombe
la vilabu bingwa barani Ulaya mara tano.
Aidha, Milan haijawahi kushinda
Taji la Seria A tangu mwaka 2011 na imemaliza katika nafasi ya 7, 10 na 8
katika misimu mitatu iliyopita.
Kwa sasa inashikilia nafasi ya 6 katika ligi kuu, alama 20 nyuma ya vinara Juventus.
No comments :
Post a Comment