Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya
Bibi Mariam Mtunguja akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano kati ya
kikosi kazi cha Kitaifa cha kunusuru ikolojia ya mto Ruaha pamoja na
Wananchi wa Kata ya Madibira wilayani Mbarali Mkoani Mbeya.
Sehemu ya Wananchi waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia kwa makini mkutano huo.
………………….
Halimashauri ya Wilaya ya
Mbalari imeagizwa kuhakikisha ng’ombe wote wa Wilaya hiyo wanawekewa
chapa ili kurahisisha kuweza kujua ng’ombe wote wa Wilaya hiyo. Pia
kila
mfugaji awe na ng’ombe wasiozidi arobaini tu ili kuweza kuzuia
uharibifu wa mazingira uanaosababibshwa na mifugo wengi kupita kiasi.
Katika maagizo hayo pia Halimashauri ya Wilaya ya Mbarali imetakiwa
kushirikiana na Wananchi wake kujenga malambo ya kunyweshea mifugo ili
kuepuka uharibifu mkubwa wa mazingira unaosababishwa na kuingizwa kwa
mifugo katika mto Ndembela kwa ajili ya kunywa maji.
Maagizo hayo yametolewa na
Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha kunusuru Mto Ruaha ambaye pia
ni Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais,
Bwana Richard Muyungi alipokua akiongea na Wananchi wa kata ya Madibira
wakati wa mkutano na Wananchi juu ya kujua na kufahamu changamoto
mbalimbali zinazosababaisha uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya
maji katika mito inayozunguka Mto wa Ruaha Mkuu ukiwemo mto Ndembela.
Akiongea katika Mkutano huo
Bwana Muyungi pia ameahaidi kushughulikia Wawekezaji ambao siyo
waaminifu wanaotumia maji bila kibali cha Serikali au wale ambao
wanazidisha kiwango cha uchukuaji maji tofauti na kile kilichoanishwa
katika kibali . Alisema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais inaratibu na
kuhakikisha rasilimali zote zilizopo Nchini zinatumika kwa usahihi .
Akijibu hoja hizo Mhe. Diwani wa
Kata ya Madibira kwa niaba ya Mkurugenzi aliahidi Halimashauri hiyo
kuyafanyia kazi mambo yote waliyoagizwa kuyafanya. Aliongeza kuwa
atasimamia yote na pia atashirikiana na Wananchi wa Madibira
kuhakikisha maagizo yote yanapatiwa ufumbuzi.
Baada ya Mkutano huo pia Wajumbe
wa Kikosi kazi hiko walipata fursa ya kutembelea shamba la mpunga la
chama cha Wanaushirika Madibira (MAMCOS) kwenda kujionea shughuli
mbalimbali za utunzaji wa maji kwa ajili ya kilimo zinavyofanyika.
Akiongea baada ya kutembelea shamba hilo la hekta 3000, Katibu Tawala wa
Mkoa wa Mbeya Bibi Mariam Mtunguja aliwapa agizo la kuweka geji
itakayodhibiti kiasi cha maji yanayotoka shambani baada ya matumizi ya
umwagiliaji kufanyika. Pia wametakiwa kutengeneza miundo mbinu
shambani ili kuwezesha barabara ya shambani hapo kupitika kwa urahisi na
maji kutomwagika hovyo. Pia kusafisha shamba lao mara moja kuondoa
nyasi na magugu yalioota kwenye mifereji ya kupitishia maji shambani
hapo.
Kikosi hiko cha Kitaifa cha
kunusuru ikolojia ya Mto Ruaha Mkuu kiliundwa na Makamu wa Rais wa
Tanzania kikijumuisha Wajumbe kutoka Idara na Taasisi mbalimbali za
Serikali. Kikosi kazi hiko kimegawanyika katika makundi matatu (Iringa,
Mbeya na Njombe.
No comments :
Post a Comment