Harakati
za marafiki wa Elimu,ni muunganiko wa wananchi mmoja mmoja ,makundi na
asasi ,taasisi zenye mapenzi na nia ya kuona kunakuwepo maendeleo chanya
katika michakato ya utoaji na usimamizi wa elimu nchini.
Harakati
hizo zilianza mwaka 2003 kwa utaratibu wa karibu wa asasi ya hakielimu
hadi sasa harakati hizi zina wanachama takribani 40,000 walioenea pande
zote za nchi wakiwakirisha makundi mbali mbali ndani ya jamii ,walimu
,wanafunzi,wanasiasa,wafanyakazi wa umma ,wazazi na kina mama.
Tangu
kuanzishwa kwa harakati hizo marafiki wamekuwa chachu katika
uhamsishaji jamii kushiriki katika shughuli za maendeleo ya elimu popote
pale walipo.Aidha wamekuwa nyenzo kuu katika kuchangia uwajibikaji wa
watendaji na wadau mbali mbali ili kuongeza na kuboresha utoaji wa
huduma kwa watu wao.
Ili
kuboresha utendaji kazi na ushiriki wa Marafiki katika shughuli za
elimu na utawala bora ,Asasi ya HakiElimu kwa kushirikiana na wadau
wengine wa Elimu imekuwa ikiwajengea uwezo Marafiki kupitia Mafunzo
mbali mbali na upatikanaji wa taarifa mbali mbali ambazo ni za muhimu
katika sekta ya Elimu.
Kutokana
na hali hiyo Wadau wa mtandao wa marafiki wa elimu Mkoani
Geita,wamekutana na kutoa taarifa ya majumuisho ya ufuatiliaji wa
uwajibikaji wa Jamii huku wakibainisha changamoto kubwa ambazo
wamekutana nazo ni upungufu wa walimu kwa baadhi ya shule zina walimu
wengi ilihali nyingine zina upungufu mkubwa .Sera ya elimu na Mafunzo
imetoa mwongozo kuwa mwalimu mmoja anatakiwa kuhudumia wanafunzi
arobaini na tano.
Akielezea
hali ya elimu mratibu wa Marafiki wa Elimu Mkoa wa Geita,Ayubu
Bwanamadi alisema tatizo la walimu kuwa wachache ni tatizo kubwa ambalo
linaendelea kudidimiza elimu kwani katika darasa nunakuta mwalimu mmoja
anafundisha zaidi ya wanafunzi 150 hadi 200 ambapo ni kinyume na sera ya
Elimu.
Meneja
wa idara ya ushiriki na uwajibikaji jamii Pius Makomelelo ,ametoa
mapendekezo ambayo yataboresha elimu ni pamoja viongo kupatiwa elimu
,lakini pia halmashauri zilizopo Mkoani Hapa kuwekeza kwenye mafunzo
ya Tehama.
Aidha
kwa Upande wake Lusenga Robart Manjale Kutoka Taasisi Ya CODERT
ameelezea masikitiko yake kutokana na hali ilivyo ya mlundikano wa
wanafunzi ambapo alitoa ushauri kwa wazazi na walezi kuchangia swala
la elimu na kuacha kusubilia serikali ifanye shughuli hiyo.
Akimwakilisha
katibu tawala wa Mkoa wa Geita,Elysalver Nkanga amesema kuwa
wataakikisha wanashirikiana na wadau wa Elimu kuboresha zaidi elimu
Mkoani Humo.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.
No comments :
Post a Comment