Mwenyekiti
wa Soko la Kimataifa la Samaki la Ferry, Ali Bunda akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam juzi wakati akitoa
taarifa ya kupungua kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika soko
hilo, baada ya kupata mafunzo kutoka Shirika la Equality for Growth
(EfG). Bunda alilitaja eneo la Lebanon katika soko hilo kuwa ni hatari kwa ukatili wa kijinsia hasa kwa watoto.
Katibu Mkuu wa Soko la Temeke Sterio, Omari Mangilile, akizungumzia kupungua kwa ukatili katika soko hilo.
Mkuu
wa Ulinzi na Usalama wa Soko la Temeke Sterio AP 1248 Koplo Chaurembo
Shomari, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es
Salaam jana, kuhusu kampeni zilizofanywa na Shirika la Equality for
Growth (EfG) za kupinga ukatili wa jinsia katika soko hilo kuwa
zimesaidia kupunguza makosa hayo ambapo kwa mwezi Septemba mwaka jana
yalikuwa 21 lakini sasa hakuna kabisa.
Mfanyabiashara katika Soko la Temeke Sterio, Robert Kalawila akizungumza na wanahabari.
Mwezeshaji Sheria Soko la Ferry, Fatma Ally akizungumza.
Mfanyabiashara katika Soko la Temeke Sterio, Mariam Juma ‘maarufu Mama Kondo’ akizungumzia kupungua kwa vitendo hivyo.
Mwezeshaji
wa kisheria katika Soko la Temeke Sterio, Augenia Gwamakombe
(katikati), akizungumza. Wengine ni wafanyabiashara wenzake.
Mfanyabiashara Tamasha Amri akizungumza.
Mfanyabiashara katika Soko la Temeke Sterio, Vicky
Mbogela akichangia jambo.
Mfanyabiashara, Lushenia Emanuel akijieleza kwa wanahabari.
Muonekano wa Soko la Samaki la Kimataifa la Ferry.
Na Dotto Mwaibale
ENEO la
Lebanon katika Soko la Kimataifa la Samaki la Ferry jijini Dar es
Salaam limeelezwa kuwa ni kinara kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia
hasa kwa watoto.
Hayo
yalielezwa na Mwenyekiti wa soko hilo Ali Bunda alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati akitoa taarifa ya
kupungua kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika soko hilo baada ya
kupata mafunzo kutoka Shirika la Equality for Growth (EfG).
“Vitendo
vya ukatili wa kijinsia vimepungua kwa kiasi kikubwa katika maeneo
mengine ya soko letu lakini changamoto kubwa ipo eneo la Lebanon huko
ukipita usiku unaweza kulia kutokana na vitendo vinavyofanyika” alisema
Bunda.
Alisema
katika eneo hilo kila vitendo vichafu vimekuwa vikifanyika kwani hivi
karibuni kuna mwanaume mmoja alikamatwa baada ya kubambwa akimnajisi
mtoto wa kiume lakini alipofikishwa kituo cha polisi mtoto huyo aliomba
mwanaume huyo asipelekwe mahakamani kwani alikuwa ni msaada mkubwa kwake
kutokana na kupewa fedha za chakula na mahitaji mengine.
“Kauli
ya mtoto huyo ilimshitua kila mtu aliyekuwepo kituoni hapo ambapo pamoja
na kuomba aachiwe polisi waliendelea kumshikilia ili sheria ichukue
mkondo wake” alisema Bunda.
Katibu
Mkuu wa Soko la Temeke Sterio, Omari Mangilile alisema ushirikiano baina
ya wafanyabiashara, viongozi wa soko pamoja na Shirika hilo na Jeshi la
Polisi Kituo cha Chang’ombe kumesaidia kupunguza vitendo vya ukatili wa
jinsia katika soko hilo.
Mkuu wa
Ulinzi na Usalama wa Soko la Temeke Sterio AP 1248 Koplo Chaurembo
Shomari alisema kampeni zilizofanywa na EfG kupinga ukatili huo
zimesaidia kupunguza makosa hayo ambapo kwa mwezi Septemba mwaka jana
yalikuwa 21 lakini hadi kufikia sasa yamepungua na kufikia mawili na
katika baadhi ya miezi mingine yakiwa hayapo kabisa.
No comments :
Post a Comment