Na Masanja Mabula –Pemba
MJUMBE wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman ameuagiza Uongozi wa Chama Chama Mapinduzi (CCM) Tawi la Kangagani Wilaya ya Wete kushirikiana katika kazi za ukarabati wa Ofisi za Tawi hilo lililozeluwa na upepo ili ukamilike kwa wakati .
Amesema
kila mwanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM katika Tawi hilo anapaswa
kushiriki kikamilivu katikia kufanikisha ukarabati wa Tawi lao kwa kuchangia misaada mbali mbali ya hali na mali ikiwa ni pamoja na nguvu kazi .
Akizungumza
baada ya kufanya ziara ya kutembelea Tawi hilo lenye Historia ndevu ya
Chama hicho Kisiwani Pemba , Mjumbe huyo wa Kamati ya Siasa ambaye pia
ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba amewaomba wanaCCM kuwa wazalendo na chama chao kwa kushiriki kazi kwa kujitolea .
Amesema
pamoja na wahisani wengine kutoa michango yao lakini ni vyema wanachama
wa chama cha Mapinduzi wa Tawi kuguswa na tukio na kujitolea kwa hali
na mali kuhakikisha linaezekwa .
“Pamoja
na wahisani kutoa michango yao kukarabati tawi hili , lakini kila
mwanachama anapaswa kuguswa , hivyo ni lazima kujitolea kuchangia
ukarabati wake kwani linahostoria kubwa katika ukombozi wa Visiwa vya Zanzibar ”alisisitiza.
Aidha
Mjumbe huyo wa kamati ya Siasa amesema Serikali ya Mkoa wa Upande wake
itashirikiana na wanachama wa Tawi hili katika ukarabati wake ili
ukamilike kwa wakati na kutoa fursa kwa wanachama kuendesha shughuli zao
za chama wakiwa sehemu tulivu .
Kwa
upande wake Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Wete ambaye pia
ni Mkuu wa Wilaya hiyo Rashid Hadid Rashid amewataka wana CCM wa tawi
hilo kutambua kwamba ukarabati wa tawi hilo utafanyika na kukamilika kwa wakati muafaka .
Amesema
yeye binfasi pamoja na Serikali ya Wilaya watasimamia ili kuona
wanachama wa CCM kwa kila mmoja anakuwa msitari wa mbele katika kutoa
michango yake .
Katibu
wa Tawi hilo Hamad Said amesema kuwa kuezeliwa kwa tawi hilo
kumerudishwa nyuma harakati za maandalizi ya uchaguzi wa chama kutokana
na kukosekana sehemu ya kuwatanisha wanachama wote.
Ameeleza
kwamba pamoja na changamoto hiyo , lakini uongozi wa chama Tawi
umefanya juhudi za makusudi kukamilika ukabarati huo kabla ya kuanza
mchakato wa uchaguzi wa ndani ya chama .
“Tunaendelea
kupokea michango na misaada kutoka sehemu mbali mbali , na tunakusudia
kukamilika ukabarati huu kabla ya kuanza mchakato wa uchaguzi wa ndani
ya chama licha ya kwamba kwa wanachama wamekosa sehemu ya kukaa na
kupanga mipango yao ”alieleza.
Tawi la CCM Kangagani limezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua na kusababisha baadhi ya kuta za jengo hilo kupasuka .
No comments :
Post a Comment