Mkurugenzi wa kituo cha mazoezi
ya Bodyline Health &Fitness, Abbas Jaffer Ali (katikati) akiongea
na waandishi wa habari wakati akitangaza tamasha la michezo
linalotarajiwa kufanyika Aprili 22, 2017 Mayfair jijini Dar es Salaam.
Pembeni ni Katibu Mkuu – Shirikisho la Watunisha Misuli Tanzania,
Francis Mapugilo (kulia) na mwalimu wa mazoezi.
Kituo
cha mazoezi cha Bodyline Health& Fitness kimeandaa tamasha la
mazoezi litakalofanyika kesho jumamosi Mayfair Msasani jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza
mkurugenzi wa Bodyline Health& Fitness, Abbas Jaffer Ali alisema
kuwa lengo la tamasha hilo ni kuwajenga watanzania wapende kufanya
mazoezi ili kuimalisha afya zao.
Aliongeza
kuwa katika tamasha hilo kutakuwa na michezo mbali mbali ikiwemo
shindano la kutunisha mishuli, kuogelea na viungo vya mwili.
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano.
Katibu Mkuu – Shirikisho la
Watunisha Misuli Tanzania, Francis Mapugilo (katikati) akisisitiza
watzania kujitokeza kwa wingi kushiriki mazoezi.
Baadhi ya washiriki wa mchezo wa kutunisha misuli wakionyesha umahili wao.
No comments :
Post a Comment