Wednesday, March 1, 2017

WAZIRI NAPE NNAUYE ATEUA KAMATI YA KUHAMASISHA USHINDI KWA SERENGETI BOYS GABON 2017


images
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ameteua Kamati Maalum ya Hamasa kuelekea Mashindano ya AFCON chini ya umri wa miaka 17 yatakayofanyika mwezi May 2017 nchini Gabon ambapo Tanzania inawakilishwa na Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya  Vijana (Serengeti Boys).
Kamati hiyo ya watu kumi(10) itaongozwa na Mwenyekiti Charles Hillary kutoka Azam Tv na
Katibu wake Selestine Mwesigwa ambaye pia ni katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wajumbe wa kamati hiyo ni Dkt Hassan Abass Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ruge Mutahaba Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group, Hoyce Temu Mrembo wa Tanzania mwaka 1999, Maulid Kitenge Mtangazaji kutoka EFM, Beatrice Singano Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania, Erick Shigongo Mkurugenzi wa Global Publishers na wasanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba na Naseeb Abdul (Diamond Platinumz).
Lengo kuu la Kamati hii ni kuhamasisha watanzania kuiunga mkono Timu ya Serengeti Boys na juhudi za Serikali katika kuhakikisha wanarudi na ushindi katika mashindano hayo.
Imetolewa na
Zawadi Msalla       
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
28/02/2017

No comments :

Post a Comment