Mfanyakazi wa kampuni ya Zantel
-Zanzibar Kassim Bakari Zuberi akichangia damu wakati wa zoezi
lililowahusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa upande wa Zanzibar ikiwa
ni njia ya kuokoa maisha ya watanzania wenye uhitaji mkubwa wa huduma
hiyo. Zoezi hilo limefanyika jana mjini Unguja. Kushoto ni ofisa kutoka
Mpango wa Taifa wa Damu Salama-Zanzibar Gabriel Laurent.
Mfanyakazi wa kampuni ya Zantel
-Zanzibar Mohamme Ali akichangia damu wakati wa zoezi lililowahusisha
wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa upande wa Zanzibar ikiwa ni njia ya
kuokoa maisha ya watanzania wenye uhitaji mkubwa wa huduma hiyo. Zoezi
hilo limefanyika jana mjini Unguja. Kushoto ni Khairia Ali Hamad,
mtoaji damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama-Zanzibar.
Afisa mdhibiti wa Rasilimali watu
wa kampuni ya Zantel -Zanzibar Said Habibu akichangia damu wakati wa
zoezi lililowahusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo ikiwa ni njia ya
kuhamasisha jamii kuchangia damu kwa hiari. Zoezi hilo limefanyika jana
mjini Unguja. Kushoto ni Khairia Ali Hamad, mtoaji damu kutoka Mpango wa
Taifa wa Damu Salama-Zanzibar.
Mfanyakazi wa kampuni ya Zantel
-Zanzibar Salum Habib Mohammed akichangia damu wakati wa zoezi
lililowahusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa upande wa Zanzibar ikiwa
ni njia ya kuokoa maisha ya watanzania wenye uhitaji mkubwa wa huduma
hiyo. Zoezi hilo limefanyika jana mjini Unguja. Kushoto ni Khairia Ali
Hamad, mtoaji damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama-Zanzibar.
Mkurugenzi wa Ofisi Kuu ya Kampuni
ya Zantel-Zanzibar Mohamed Musa Baucha akijiandaa kuchangia damu wakati
wa zoezi la uchangiaji damu kwa hiari lilloandaliwa na kampuni hiyo
ikiwa ni njia ya kuhamasisha jamii kuchangia damu kwa hiari. Zoezi hilo
limefanyika jana mjini Unguja. Kushoto ni ofisa kutoka Mpango wa Taifa
wa Damu Salama-Zanzibar Gabriel Laurent.
………………………………………….
Katika kuisaidia benki ya damu
hapa nchini, wafanyakazi wa Zantel-Zanzibar wamejitokeza kwa wingi na
kujitolea kuchangia damu katika kuendeleza mwitikio huo kwa jamii
ulioanzishwa na Kampuni hiyo wiki iliyopiata katika makao makuu yake
jijini Dar es Salaam.
Zoezi hili ambalo linaratibiwa na
Kitengo cha uwajibikaji kwa jamii (CSR) cha Kampuni hiyo, limelenga
kusambaza upendo kupitia shughuli hii ya uchangiaji damu ili kuiwezesha
benki ya damu sambamba na kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu.
Shughuli hiyo ya uchangiaji
iliyofanyika katika makao makuu ya Ofisi za Zantel-Zanzibar, ilishuhudia
mwitikio mkubwa kutokana na wingi wa wafanyakazi wa Zantel kujitokeza,
pamoja na baadhi ya wananchi wakishiriki kuchangia damu.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo
la uchangiaji damu, Mkurugenzi wa Ofisi kuu ya Zantel-Zanzibar, Bw.
Mohamed Musa Baucha aliwashukuru watu wote walioshiriki na kutoa rai kwa
makampuni mbalimbali pamoja na wananchi kuwa tayari kujitolea kwenye
shughuli kama hizo wanapotakiwa kufanya hivyo.
“Tunayo furaha kwa mwitikio huu wa
kukubali kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu kwa kuonyesha upendo
hususan wafanyakazi wa Zantel Zanzibar. Niwaombe muendelee na moyo huu
huu wa kujitolea pindi mnapohitajika kushiriki kwenye shughuli nyingine
kama hizi,”alisema.
Kwa upande wake, Afisa Uhamasihaji
wa Mpango wa damu salama Zanzibar Bw. Omar Said Omar alisema kwamba
zoezi la uchangiaji damu limefanyika kwa mafanikio makubwa na
amefurahishwa na moyo wa kujitolea ulioonyeshwa na wafanyakazi wa
Zantel-Zanzibar. Hata hivyo aliongeza kuwa, bado mahitaji ya damu ni
makubwa ikilinganishwa na kiwango kilichokusanywa ambapo kwa mwaka huu
wa 2017 walijiwekea lengo la kukusanya chupa 12,000.
Alisema kwamba shughuli ya
kukusanya damu ni zoezi endelevu la kujitolea, benki ya damu imekuwa
ikiomba makampuni na jamii kwa jumla kutambua umuhimu wa kuchangia damu
ili kuokoa maisha ya wananchi.
“Ni watu wachache sana ambao
wamekuwa wakijitokeza kuchangia damu, hivyo tunaamini kuwa zoezi hili
litaendelea kuwahamasisha watu wengi kujitokeza kushiriki,” alisema.
No comments :
Post a Comment