Frank Mvungi-Maelezo
Watanzania wametakiwa kujitolea
kuchangaia Damu ili kuwasaidia wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji wa moyo
wanaohitaji kuongezewa damu wakati wa kupatiwa mat
ibabu.
Kauli hiyo imetolewa na
Mkurugenzi wa Upasuaji wa Moyo na Daktari Bingwa wa Moyo Dkt. Bashir
Nyangasa kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa
Mkutano na
Waandishi wa Habari uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
“Tunatarajia kuwa na kambi maalum
ya matibabu ya moyo kwa watoto itakayoanza tarehe 3/4/2017 hadi tarehe
7/4/2017 ambapo Taasisi yetu itashirikiana na Madaktari Bingwa kutoka
Taasisi ya Healinga Little ya London Uingereza.”Alisisitiza Dkt.
Nyangasa
Akifafanua Nyangasa amesema kuwa
wagonjwa 12 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika kipindi hicho kwa
ushirikiano na Madaktari hao kutoka Taasisi ya Healing Little ya London
Uingereza.
Kufuatia upasuaji huo Dkt.
Nyangasa amewaomba wananchi kuendelea kuchangia damu ili kusaidia
kuokoa maisha ya wale wanaohitaji kuongezewa damu.
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete
imekuwa Moja ya Taasisi Bora katika ukanda wa Afrika mashariki na Kati
katika kutoa matibabu moyo kwa wagonjwa kutoka hapa nchini na katika
mataifa mbalimbali yanayoizunguka Tanzania.
Upatikanaji wa damu yakutosha
imekuwa moja ya changamoto zinazoikabili Sekta ya afya kutokana na
mwitikio mdogo wa wananchi kujitolea damu ili kusaidia wale wenye
uhitaji hivyo ni wajibu wa kila mtanzania kuunga mkono juhudi za Taasisi
ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika kuhamasisha wananchi kujitolea
kuchangia damu
No comments :
Post a Comment