Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akizungumza na
hadhira (haipo katika picha) katika hafla ya Uzinduzi wa maonyesho ya
kwanza ya Tamhiliya ya kichina inayoitwa “Mfalme Kima” kwa lugha ya
Kiswahili uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel (wa pili kushoto)
akizungumza na Naibu Waziri wa Utangazaji wa Serikali ya Jamhuri ya Watu
wa China Mhe.TONG GANG (wa kwanza kulia) kabla ya Uzinduzi wa maonyesho
ya kwanza ya Tamhiliya ya kichina inayoitwa “Mfalme Kima” kwa lugha ya
Kiswahili uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa uzalishaji wa
vipindi vya Luninga Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bibi Suzan
Mungy akizungumza na hadhira (haipo katika picha) akitoa maelezo mafupi
kuhusu Shirika hilo linavyoshirikiana na Serikali ya China katika
hafla ya Uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya Tamhiliya ya kichina
inayoitwa “Mfalme Kima” kwa lugha ya Kiswahili uliofanyika leo Jijini
Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel pamoja na Naibu
Waziri wa Utangazaji wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Mhe.TONG
GANG wakikata utepe kuashiria Uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya
Tamhiliya ya kichina inayoitwa “Mfalme Kima” kwa lugha ya Kiswahili
uliofanyika
Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel pamoja na Naibu wa
Utangazaji wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Mhe.TONG GANG
(katikati waliosimama) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
waandaaji na washiriki wa Uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya Tamhiliya
ya kichina inayoitwa “Mfalme Kima” kwa lugha ya Kiswahili uliofanyika
leo Jijini Dar es Salaam.
………………
Na Shamimu Nyaki-WHUSM
Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amewaomba
Wataalamu wa lugha ya Kichina hapa nchini kutafsiri Filamu za Kiswahili
kwa
lugha ya kichina ili zipate soko nchini China.
Prof. Elisante Ole Gabriel
ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa anazindua Maonyesho ya
kwanza ya Tamthiliya ya kichina inayoitwa “Mfalme Kima” iliyotafsiriwa
kwa lugha ya Kiswahili ambapo amesema kuwa njia nzuri ya kufikisha
ujumbe kwa watanzania katika filamu za kichina ni kutumia lugha ya
Kiswahili.
“Njia rahisi ya kufikisha ujumbe
kwa watu wote ni kutumia lugha mtambuka katika tamthiliya zetu hii
itasaidia sana kukuza uhusiano wetu na Jamhuri ya Watu wa China”,Alisema
Prof.Ole Gabriel.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Uzalishaji wa Vipindi vya Luninga Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC)
Bibi Suzan Mungy ameelza kuwa ushirikiano wa shirika hilo na Kampuni ya
Star Times ambayo ndio waandaji wa Tamthiliya hiyo umeleta mafanikio
makubwa ikiwemo kuongezeka kwa watazamaji wanaopenda tamthiliya za
kichina zenye tafsiri ya lugha ya Kiswahili zinazooneshwa katika luninga
hiyo.
“Ushirikiano wetu unazidi
kuimarika na tunaamini utaleta mafanikio makubwa zaidi kwetu sote katika
kutoa elimu na Burudani kupitia Tamthiliya na vipindi vingine
vinavyopatikana katika visimbuzi vya Star Times”,Alisema Bibi Suzan.
Uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya
Tamthiliya ya Kichina “Mfalme Kima” kwa lugha ya Kiswahili imezinduliwa
leo Jijini Dar es Salaam ambapo maudhui yake yanatoa elimu pamoja na
Burudani.
No comments :
Post a Comment