Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya
Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo ambaye kachaguliwa kuwa MUWEKA HAZINA
wa Wakurugenzi nchini
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Ndg Kiomoni Kibamba, ambaye kachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Wakurugenzi nchini
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Ndg Anne Claire Shija (Kushoto) ambaye kachaguliwa kuwa katibu wa Wakurugenzi nchini
Na Mathias Canal, Dodoma
Wakurugenzi wa Halmashauri za
Wilaya na Manispaa kote nchini kwa kauli moja wameridhia na kuwachagua
viongozi watakaowawakilisha katika kufikisha changamoto zao mbalimbali
katika ngazi za juu ili kupungunza uwasilishaji wa kila Mkurugenzi
kufikisha changamoto zake ngazi za juu.
Uchaguzi huo umefanyika hii Leo
katika ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma kwa maridhiano ya Wakurugenzi wote
kwa asilimia 100% ya kura zote.
Uchaguzi huo umejili Mara baada
ya kumalizika kikao cha kazi kilichoongozwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Eng Musa Iyombe
kilichohudhuriwa na Wakurugenzi wote 185.
Wakurugenzi hao wamefanya
uchaguzi kwa nafasi nne ambazo ni Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti
sambamba na Katibu pamoja na Muweka Hazina.
Wakurugenzi waliochaguliwa katika nafasi hizo ni
1. Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Ndg Kiomoni Kibamba, ambaye kachaguliwa kuwa Mwenyekiti
2. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Ndg Rachel Chuwa ambaye kachaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti.
3. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Ndg Anne Claire Shija, ambaye kachaguliwa kuwa katibu. Na
4. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
Ndg John Lipesi Kayombo ambaye kachaguliwa kuwa MUWEKA HAZINA
Ndg John Lipesi Kayombo ambaye kachaguliwa kuwa MUWEKA HAZINA
Wakizungumza kwa nyakati tofauti
Mara baada ya uchaguzi huo kumalizika Viongozi hao waliochaguliwa
wameeleza namna bora ya kuhumiza uwajibikaji kwa Wakurugenzi wote
sambamba na kuwawakilisha vyema kufikisha changamoto zao kwa ngazi za
juu.
Wameueleza mtandao wa www.wazo-huru.blogspotm.com kuwa
imani kubwa waliyopatiwa na Wakurugenzi wote nchini ya kuwachagua kuwa
wawakilishi wao ni kubwa hivyo wana kila sababu ya kuitumikia kwa weledi
na usawa.
“Kupitia Wawakilishi hao
waliochaguliwa Wakurugenzi nchini wataraji utendaji uliotukuka na
uwakilishi unaostahili kulingana na changamoto zinazowakabili katika
maeneo yao” Alisema MD Kayombo John L.
No comments :
Post a Comment