Mwenyekiti
wa The Desk & Chair Foundation tawi la Tanzania Sibtain Meghjee
akimtwisha ndoo ya maji milembe Kuhamwa, Mwenyekiti wa Kiyongoji cha
Mwashileko katika Kijiji cha Kasololo wilayani Misungwi Mwanza, ikiwa ni
ishara ya kukabidhi kisima cha maji safi na salama kati ya saba
vilivyochimbwa na taasisi hiyo kwa gharama ya sh. 21 milioni.
Mmoja
wa wakazi wa Kijiji cha Kasololo katani humo katika Wilaya ya Misungwi
aichota maji baada ya kukabidhiwa kisima cha maji kilichochimbwa na
taasisi ya The Desk & Chair Foundation ili kuwapunguzia ya kero ya
maji inayowakabili kwa muda mrefu.
Mwenyekiti
wa The Desk & Chair Foundation Sibatain Meghjee (kushoto nyuma ya
pump ya maji) akizungumza na wananchi baadhi wa Kijiji cha Kasololo
katika Wilaya ya Misungwi baada ya kuwakabidhi moja ya visima
vilivyochimbwa na taasisi hiyo hivi karibuni.
Mmoja
wa wananchi wa Kitongoji cha Isuka akizungusha mkono wa pump ya
kusukuma maji katika moja ya visima saba vilivyochimbwa na Taasisi ya
Desk & Chair Foundation na kuvikabidhi kwa wananchi wa kitongoji
hicho katika Kijiji cha Kasololo Wilaya ya Misungwi Mwanza.Anayeshuhudia
ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo Sibtain Meghjee (kushoto).
Mwenyekiti wa The Desk &
Chair Foundation Sibatain Meghjee (kulia) akitoa maelezo kwa wananchi wa
kitongoji cha Iwelimo jinsi ya kutumia paump ya kusukama maji katika
moja ya visima vilivyotolewa msaada kwa wananchi wa vitongoji vya Kijiji
cha Kasololo katika Wilaya ya Misungwi hivi karibuni ili kuwasidia
kuondokana na adha ya maji.
Wananchi
wakimsikiliza mfadhili aliyechimba visima vya maji Sibatin Meghjee
Mwenyekiti The Desk & Chair Foundation ili kukabiliana na kero ya
maji kijijini Kasololo Misungwi hivi karibuni.
Mkazi
wa kitongoji cha Iwelimo Rahel Yuda akizungusha mkono a pump ya
kusukuma maji baada ya kukabidhiwa kisima na mwenytkiti wa The desk
& Chair Foundation sibtain Meghjee anayeshuhudia kulia.kisima hicho
ni moja kati ya saba vilivyombiwa na taasisi hiyo katika Kijiji cha
Kasololo wilayani Misungwi viwasaidie kuondokana na kero ya maji.
Shoma
Motomkali wa kitongoji cha Iwelimo akichota maji akiwa na mwanaye
mgongoni baada ya kitongpoji hicho kukabidhiwa kisima cha maji kati ya
vitatu vilivyochimbwa kenye kitongoji hicho na The Desk & Chair
Foundatio.kujlia ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo Sibtain Meghjee.
Afisa
Mtendaji wa kijiji cha Kasololo Mabula Bukanu akimtwisa ndoo ya maji
Susane Faustine ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kisima xcha maji kwenye
itongoji cha Iwelimo hivi karibuni.kisima hicho ni moja ya saba
vilivyochimbwa na taasisi ya The Desk & Chair foundation/
Mwalimu
Mkuu msaidizi wa Shule ya Sekondari Kasololo Rahim Ayub akijaribu
kuzungumsha mkono wa pump ya kusukuma maji katika kisima kilichochimbwa
kwenye Kitongoji cha Iwelimo katika Kijiji cha Kasololo wilayani
Misungwi.Kisima hicho kitanufaisha hule hiyo yenye wanafunzi 320.Kushoto
ni Sibtain Meghjee Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation
iliyochimba na kufadhili visma hivyo kwa gharama ya sh. 21 milioni.
………………….
Picha zote na Baltazar Mashaka
NA BALTAZAR MASHAKA,MISUNGWI
KERO
ya uhaba wa maji iliyokuwa ikiwakabili wananchi zaidi ya 1000 wa
vitongoji vitano vya Kijiji cha Kasololo wilayani Misungwi mkoani Mwanza
na kusababisha ndoa nyingi kuvunjika pamoja na migogoro kwenye familia,
imetatuliwa baada ya Taasisi ya The Desk & Chair Foundation
kuchimba na kujenga visima saba.
Mwenyekiti
wa The Desk & Chair Foundation tawi la Tanzania Sibtain Meghjee
akikabidhi visima hivyo vilivyogharimu sh 21 milioni alisema walisitisha
ujenzi wa Msikiti (nyumba ya ibada ) ili watatue kero ya maji kwa
kuwapa wananchi huduma ya maji itakayowanufaisha watu zaidi ya 1200 kwa
matumizi ya kibinadamu.
Alisema
visima vimekabidhiwa ili kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Bi. Fatma AS.
mjukuu wa Mtume Mohamed S.A.W.ambaye alifanya kazi kubwa ya kusaidia
jamii lakini pia miradi ya kijamii inayofadhiliwa na waumini wa
madhahebu ya Shia Ithna Asheri, kwenye maadhimisho hayo ilikabidhiwa
huko Kwimba Mwanza na Kondoa mkoani Dodoma na maeneo mengine nchini.
“Dini
ya Kiislamu licha ya kupakaziwa mambo ya ovyo na kuhusishwa na ugaidi
ni nzuri na haya yanayofanywa na The Desk & Chair Foundation ndiyo
uislamu wenyewe.Tumewapunguzia kero ya maji wananchi wa Kasololo na siri
ya kudumu kwa visima hivi matunzo ni muhimu lakini pia tengeni maeneo
yasiyo na migogoro kwa ujenzi wa maombi mapya ya visima,”alisema
Sibtain.
Wakizungumza
jana baada ya kukabidhiwa visima hivyo saba vya maji safi na salama
vilivyochimbwa katika vitongoji vitano vya vya Isuka, Bugumo,
Mwashileko,Iwelimo na Kasololo baadhi ya wananchi walisema tatizo hilo
la ukosefu wa maji lilikuwa linawakabili kwa muda mrefu litapungua
ingawa bado changamoto ipo.
Petro
Mbogo mkazi wa kitongoji cha Iwelimo kilichopata visima vitatu alisema
kero ya maji ilisababisha migongano kwenye jamii, migogoro katika
familia pamoja na ndoa nyingi kuvunjika kutokana na akina mama kukesha
wakisubiri kuteka maji usiku kwenye vyanzo vya asili ambavyo hukauka
wakati wa kiangazi.
“Maji
yalikuwa kero kwa miaka mingi katika kijiji chetu na wakati wa kiangazi
tulisafiri umbali wa km 5 kwenda kuchota maji ziwani.Wanawake walikuwa
wakisumbuka mno kupata maji, ndoa nyingi zilivunjika, kulizuka migongano
na migogoro kwenye familia sababu ya maji,”alisema Mbogo.
Alisema
kupatikana kwa visima hivyo sasa kutawapa wanawake fursa na muda wa
kufanya shuguli za uzalishaji pamoja na maendeleo tofauti na zamani
ambapo walipoteza muda mwingi wakitafuta maji kwa matumizi ya familia
zao na kushindwa kuzalisha.
Naye
Mariamu Jeremiah wa kitongoji cha Bugumo alisema visima hivyo vitakidhi
mahitaji ya wananchi wa vitongoji vya kijiji hicho ambao awali
walifikia hatua ya kupigana wakigombea kuchota maji kutoka kwenye visima
vya asili kwa kulowa maji (kuchota kwa kutumia kamba) huku wakilazimika
kuwaacha waume zao wamelala kwenda kutafuta maji.
“Mungu
amesikia kilio chetu cha maji japo pump ni nzito kwa watu wa umri
mkubwa,tunashukuru kwa msaada huu wa visima vya maji, maana hatukuwa
tunaoga wala kufua nguo za waume zetu, ndoa zilivunjika wanawake wengine
walipigwa na waume zao kwa kuchelewa sababu ya maji,watoto walikatishwa masomo,walikuwa hawanawi nyuso,”alisema Bi. Jeremiah.
Alidai
walilazimika kuyafuata maji ziwani umbali wa maili 5 kutokana na
kuambulia ndoo moja kwenye kisima wakichukua muda wa saa 8 kuipata huku
ndoo moja ya ujazo wa lita 18 wakiuziwa sh.500 hali ambayo kwa wananchi
wasiokuwa na ajira yalikuwa ni mateso kumudu gharama za maji kwa
familia.
Kwa
mujibu wa wakazi wa kitongoji cha Iwelimo Susan Fustine,Rahel
Yuda,Shoma Motomkali na Regina Joseph licha ya kusogezewa karibu huduma
hiyo bado wanakabiliwa na adha kubwa ya maji na hivyo waongezewe visima
vingine huku Mwalimu Mkuu msaidizi wa Shule ya Sekondari Kasololo Rahim
Ayoub akieleza kuwa walimu na wanafunzi watayatumia maji hayo kwa
mahitaji ya kibinadamu na kumwagilia miti ili kuboresha na kutunza
mazingira ya shule.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Kasololo Ruben Masasi licha ya kushukuru kwa msaada huo
ambao haukutegemewa alidai umeondoa migogoro kwenye familia zilizokumbwa
na kadhia hiyo na kunusuru ndoa zisiendelee kuvunjika lakini kutokanana
idadi ya ongezeko la watu,mahitaji yataongezeka na kuomba wasaidiwe
visima vingine.
No comments :
Post a Comment