Ubalozi wa Japan Leo tarehe 29
March, 2017 umesaini mkataba wa usd 104,135 Sawa na Tsh 230m na
Halmashauri ya Mji wa Mafinga kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Upasuaji
kwenye Hospital ya Mafinga.
Akizungumza wakati wa kusaini kwa
mkataba wa msaada huo, Balozi wa Japan hapa...
nchini Mhe. Masaharu
Yoshida alisema kwamba msaada huo ni matokeo ya Ombi la Mhe Cosato Chumi
Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini aliloliwasilisha Ubalozini mwaka
uliopita.
Aidha Mhe Balozi Yoshida alimpongeza Mbunge
huyo kwa ushirikiano alioutoa hasa katika kufuatilia katika ngazi
mbalimbali za serikali ikiwemo Wizara ya Fedha kwa ajili ya kupata
ridhaa ya kusaini mkataba wa msaada huo.
Pamoja na msaada huo, Serikali ya
Japan kupitia Ubalozi wake hapa nchini, umetoa msaada kwa Halmashauri
za Bukoba, Temeke na Chuo cha Ufundi Yombo.
Halmashauri ya Bukoba imepewa
msaada wa usd 108,025 (Tsh (238m) kwa ajili ya ujenzi wa madarasa kwenye
shule za Msingi za Nyakato na Kashozi ambazo ziliathiriwa na tetemeko
la ardhi.
Kwa upande wa Temeke wamepokea msaada wa usd 137,837 (Tsh 274m) kwa ajili ya kuboresha Jengo la Huduma ya dharura kwenye Hospital ya Rufaa ya Temeke.
Chuo Ufundi Yombo wamepokea msaada wa usd 64,499(Tsh 130m) kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya madarasa ya wanafunzi wenye ulemavu.
Kwa upande wa Temeke wamepokea msaada wa usd 137,837 (Tsh 274m) kwa ajili ya kuboresha Jengo la Huduma ya dharura kwenye Hospital ya Rufaa ya Temeke.
Chuo Ufundi Yombo wamepokea msaada wa usd 64,499(Tsh 130m) kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya madarasa ya wanafunzi wenye ulemavu.
Jumla ya usd 408,496 (Tsh 900m)
zimetolewa katika misaada hiyo inayolenga kuwasaidia wananchi ngazi za
chini yaani Grant Assistance for Grassroots Human Security Projects .
Akizungumza Mara baada ya
kusainiwa kwa mikataba ya misaada hiyo, Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato
Chumi, alimshukuru Balozi Yoshida na Serikali ya Japan kwa kuendelea
kufadhili miradi hasa inayolenga kuwafikia watu wa chini.
Aidha Chumi alimshukuru Wizara ya
Fedha kwa kuridhia kusainiwa kwa mikataba ya misaada hiyo kabla ya
kumalizika kwa mwaka wa Fedha wa Japan March 31. ‘Namshukuru Sana Mhe Dr
Philip Mpango na watendaji wake kwa jinsi ambavyo walifanya kazi usiku
na mchana kuhakikisha kuwa taratibu zote za kisheria na kikanuni
zinatimizwa kwa wakati ili mikataba hii iweze kusainiwa siku ya leo’
‘Pamoja na misaada mikubwa
kupitia ushirikiano baina ya nchi hizi mbili yaani bilateral cooperation
, bado Japan imeendelea kutoa na kufadhili miradi inayotekelezwa katika
ngazi za chini kabisa, hili ni jambo jema na tunaopokea Fedha hizi
tuzitumie kwa malengo yaliyokusudiwa’ Alisema Chumi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Mji wa Mafinga Bi Saada Mwaruka alisema kuwa msaada huo
ni ukombozi kwa watu wa Mafinga na Mufindi kwa ujumla kutokana na ukweli
kwamba Hospital hiyo inahudumia Wilaya ya Mufindi na hata Wilaya za
jirani kama Mbalari na Iringa Vijijini.
Katika kipindi cha miaka mitano
kuanzia kuanzia mwaka 2011 jumla ya usd 6.7m (Tsh 15bilioni) zimetolewa
na Serikali ya Japan maalum kwa ajili ya kufadhili jumla ya miradi
sitini (60) ya Afya, Elimu na Maji. Miradi hiyo imetekelezwa katika
ngazi za Halmashauri
No comments :
Post a Comment