Wednesday, March 1, 2017

Tigo, Ericson washirikiana kuunganisha maeneo ya vijijini Tanzania



  • Tigo na Ericson wazindua maeneo ya kwanza ya 3G katika miundombinu ya ushirikiano ya GSMA inayojielekeza  kuunganisha maeneo ya vijijini nchini Tanzania.
  • Mfumo wa Redio wa Ericsson  kwa mara ya kwanza utawapatia wateja huduma bora ya mtandao wa simu, huduma iliyo na ubora ambayo kampuni ya simu za mkononi ya Tigo  imekuwa ikiitoa kwa wateja mbalimbali.
  • Katika ushirikiano huu, kampuni ya Tigo itakuwa na asilimia 40 katika uendeshaji wa mtandao.
Ericsson (NASDAQ:ERIC) na mtandao wa simu  unaoendeshwa Tanzania Tigo  wameungana  katika kuzindua maeneo ya minara ya mfano katika maeneo ya vijijini  itakayotoa  huduma za simu kwa maeneo  ya Chiwale na Mingumbi katika mikoa  ya  Lindi  na Mtwara ambayo yamo ndani vijijini  na awali yalikuwa hayajaunganishwa.
Shughuli hiyo ni mwanzo wa miundombinu ya mfano ya kushirikiana  kunakofanywa na GSMA pamoja na Tigo, serikali ya Tanzania na waendeshaji wawili wakubwa wa mtandao wa simu kwa kuunganisha  zaidi ya watu binafsi zaidi ya milioni 13 wanaoishi sehemu za maeneo ya vijijini hapa nchini.
Miundombinu ya kushirikiana  na kuihusisha serikali  katika kupunguza kodi  katika mikoa hiyo  kunawaruhusu waendeshaji  kupunguza gharama za  kuendesha mitandao mipana katika maeneo ambayo  awali ilikuwa haifikiwi na huduma za simu.
Tigo na Ericson zimetoa nafasi katika  ushirikiano huu  kwa kuzindua  eneo la kwanza linalofanya kazi kwa kutumia mfumo wa Redio wa Ericson wa kizazi kipya wenye  viwango vingi. Seti hiyo ya suluhisho  inawezesha kuwepo kwa uwezo  unaotakiwa katika kupunguza gharama za jumla za umiliki  hadi asilimia 40 pindi eneo la suluhisho la jumla kwa uwanda mpana wa  simu wa  Ericsson utakapoanza kufanya kazi. Hii inafanya  uwekezaji unaokuwepo katika masoko  kuwa na wastani wa chini wa mapato kwa kila mtumiaji.
Suluhisho  hili litaiwezesha Tigo na washirika wake  kuweza kuyabaini  kwa urahisi maeneo yasiyo na huduma katika mkoa,  kuharakisha kuanzisha au kuboresha  uzoefu wa watumiaji wengine wa uwanda mpana wa simu ndani ya jamii hizi za vijijini.  Huu ni uzinduzi wa kwanza kibiashara kwa suluhisho hilo katika  Afrika,  Kusini mwa jangwa la Sahara.
Fundi Mkuu na Ofisa wa Teknolojia ya Habari, Jerome Albou wa Tigo Tanzania  alisema, “ndani ya Tigo ni  dira yetu kuongoza katika kupokea intaneti na mtindo wa maisha  ya kidijitali  nchini Tanzania.  Kufikiwa kwa uwanda mpana wa simu za mkononi  kutazifungua jumuia hizi za  vijijini katika huduma  ambazo awali  walikuwa hawazipati kama vile huduma ya fedha kwa njia ya simu, huduma za afya kielektroniki, elimu kielektroniki, na serikali mtandao, hivyo kubadilisha namna ambavyo watu wanacheza, kujifunza  na kufanya biashara kwa ujumla”.
Mkuu wa Ericsson Kanda ya Afrika, Kusini mwa jangwa la Sahara Jean-Claude Geha, alisema; “Sisi ni wapiga mbiu vinara wa mchango wa  Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) katika kuwezesha utambuzi wa seti mpya na za jumla  za Malengo Endelevu ya Milenia (SDGs). Washirika wetu kwa pamoja wanatafuta masuluhisho  ya kuleta faida zinazopatikana katika teknolojia ya simu za mkononi  kwa kila mtu kwa kuunda  ulimwengu  ambao ni endelevu na  jumuishi zaidi”.
Muunganiko huo mpya wa suluhisho unajumuisha; program ya Ericsson inayosimamia eneo, pamoja na program ya kudhibiti eneo, ambavyo  ni Redio 2219, Redio iIiyounganishwa na Antenna, AIR 2488, MINI-LINK 6363, MINI-LINK 6651 ambacho ni kifaa cha ndani na nyongeza mpya kwa ajili ya kuunganisha mitambo hii ya Ericsson. Hali kadhalika inajumuisha programu mpya iliyoboreshwa katika Zero Touch WCDMA na masuluhisho ya mtiririko wa watumiaji

No comments :

Post a Comment