Wednesday, March 1, 2017

TDL Imesitisha utengenezaji pombe kwa vifungashio vya plastiki


images
-Maofisa wa TFDA wakuta uzalishaji umesitishwa
Kampuni ya TDL maarufu kama konyagi imesitisha utengenezaji za pombe kwa kutumia vifungashio vya plastiki kwa mujibu wa agizo la serikali ambapo mwisho wa kusambaza pombe hizo ulikuwa jana.
Maofisa kutoka Mamlaka ya kusimamia vyakula na Madawa (TFDA) na NEMC, TRA Pamoja na POLISI wamefika kiwandani leo na kukuta hakuna uzalishaji wa vinywaji hivyo unaoendelea kama ambavyo kuna taarifa za kupotosha kwenye mitandao ya kijamii zinazoeleza kuwa TDL imekaidi agizo la serikali na imekutwa ikiendelea kufanya uzalishaji kwa kutumia vifungashio vilivyopigwa marufuku na serikali.
TDL siku zote imekuwa ikiendesha shughuli zake za kibiashara kwa kufuata miongozo na sheria za serikali kupitia taasisi zake mbalimbali hivyo haiwezi kukaidi na kuendelea na uzalishaji wa kutumia vifungashio vya plastiki wakati vimepigwa marufuku bali inajipanga kutumia teknolojia ya kutumia vifungashio vilivyotengenezwa kwa malighafi ya kioo ambavyo vina ubora  wa hali ya juu na salama kwa kuwa sio rahisi kuviigiza

No comments :

Post a Comment