Wednesday, March 1, 2017

Baraza la Madiwani Jiji la Arusha chakutana kwa Robo ya Pili


NTE1
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Athumani Kihamia akitoa maelekezo wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani
NTE2
  1. Mstahiki Meya wa Jiji Mhe. Kalisti Lazaro(kushoto) akiteta jambo na Naibu Meya wa Jiji Mhe. Viola Lazaro Likindikoki wakati wa Kikao cha Baraza.
NTE3
Madiwani na wataalam wakifuatilia kikao cha Baraza la Madiwani robo ya Pili.
NTE4
NTE5Afisa Utumishi Mkuu wa Jiji. Ndg. Baltazari Ngowi(Kushoto) akiwa na Kaimu Mwanasheria wa Jiji Fabiola Kisarika wakati wa Kikao cha Baraza.
NTE6Katibu wa Mwenezi wa CCM Arusha Mjini Gasper Kishumbua(kushoto) akiteta jambo na Katibu wa Chadema Wilaya ya Arusha Innocent Kisanyage wakati wa Kikao cha Baraza (kulia).
………………………………………………………….
Nteghenjwa Hosseah, Arusha
Kikao cha Baraza la Madiwani Jiji la Arusha kilichoketi kwa robo ya pili kwa mujibu wa kanuni kimepitisha taarifa mbalimbali za shughuli za maendeleo, kuidhinisha mapendekezo ya
Sheria ndogo za Jiji za mwaka 2006 pamoja kupokea taarifa mbalimbali kutoka kwa Taasisi za Serikali zinazotoa huduma kwa wananchi wa Jiji la Arusha.
Akifungua Kikao hicho Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Kalisti Lazaro amewataka wajumbe wa Kikao kuwa makini katika kujadili na hoja mbalimbali zilizowasilishwa katika Baraza ili kuweza kuleta Tija kwa wananchi wa Jiji na wanaotegemea kupata maendeleo kupitia vikao.
Naye Mkurugenzi wa Jiji Ndg. Athumani Kihamia alisema kwa kushirikiana na Menegiment amehakikisha kwamba maazimio yote ya vikao vya awali yamezingatiwa na miradi imetekelezwa kwa kiwango cha juu huku thamani ya Fedha ikionekana.
 Kutoka katika taasisi zilizoalikwa katika kikao hicho Mkurugenzi wa AUWSA Eng Ruth Koya alieza changamoto kubwa inayowakabili wananchi kwa sasa kuwa ni uhaba wa Maji na kusema kuwa wanategemea kuanza utekelezaji wa mradi mkubwa ambao utawezesha upatikanaji wa maji Lita Mil 200 wakati mahitaji ni Mil 94 tofauti na sasa ambapo kiasi kinachohitahjika ni Lita Mil 35 tu ambacho hakitoshelezi hata nusu ya mahitaji ya wananchi, hivyo kinachohitajika ni ushirikiano wa wadau na wananchi ili kuweka kufanikisha utekelezaji.
Akiendelea kujibu maswali ya Wah. Madiwani waliyohoji maji yanayopatikana kuwa na Chumvi Eng. Koya alisema maji ya kisima yanayopatikana Arusha kwa kiasi kikubwa yana uwekezekano wa kuwa na chumvi kidogo lakini na hayana Flouride tofauti nay ale ambayo wananchi wanadai ni matamu huwa ni ya yanatokana na Chemchem ambayo hayapatikani kwa wingi na athari zake ni kuwa na Flouride ambayo mtumiaji huwezi kuigundua kwa kunywa lakini athari zake huonekana kwenye meno nk.
Kutoka Tanesco Mhandishi wa Mipango na Ubunifu Eng.Beatus Rwegoshora alifafanua tatizo la kukatika umeme mara kwa mara kuwa Tanesco iko katika maboresho ya huduma kwa wateja nahivyo tatizo hilo litapungua na pia shirika lipo katika mpango mahususi wa kuwafanya wananchi waweze kupata taarifa zote za msingi kupitia simu za kiganjani ambapo huduma hiyo itawafanya wananchi kufuatilia na kupata taarifa kwa wakati na muda wote popote walipo.
Meneja wa Sumatra Mkoa wa Arusha Bw. Allen Mwani amesema kwa sasa Mamlaka hiyo  ipo katika upembuzi yakinifu wa mradi wa kuondoa usafiri wa daladala maarufu,  ‘Vifodi’ ambazo hazina viwango katika usafirishaji wa abiria hivyo mpango uliopo ni wadau kukaa pamoja na kuleta magari makubwa ya usafirishaji wa abiria(City Bus) katika jiji la Arusha.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala AICC Ndg. Savo Mng’ong’o aliwatoa shaka Madiwani waliolalamikia Hospital ya Kituo hicho kutopokea Kadi za Bima ya Afya (NHIF) ilihali wananchi wanahimizwa kujiunga na mfuko huu ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za matibabu kwa alifafanua kuwa huduma hiyo itarejea mwezi Oktoba.
Katika kikao hiki pia Baraza limepitia na kuidhinisha Sheria ndogo za Halmashauri ambapo sasa zitawasilishwa Mkoani kisha Tamisemi kwa ajili ya kuidhinisha kisha kuanza kutumika rasmi. Sheria hizi ni muhimu sana kwa jiji kwa kuwa zinazotumika sasa ni zile za mwaka 2003.

No comments :

Post a Comment