Sunday, March 26, 2017

TBL Group kuendelea kushirikiana na wakulima nchini


mku1
Wakulima wanahitaji kuwezeshwa kuendesha kilimo cha kisasa kama hiki ili waweze kupata  mazao ya kutosha na kuboresha maisha yao ,mpango wa TBL Group kushirikiana na wakulima utasaidia kuleta mabadiliko 
mku2
Wakulima wanahitaji kuwezeshwa kuendesha kilimo cha kisasa kama hiki ili waweze kupata  mazao ya kutosha na kuboresha maisha yao ,mpango wa TBL Group kushirikiana na wakulima utasaidia kuleta mabadiliko  hapa anaonekana mmoja wa wakulima akina mama akivuna mtama.
mku3
Mikakati madhubuti inahitajika kuwapatia wakulima nyenzo za kisasa badala ya kutumia jembe la mkono
mku4
Wakulima wanaoshirikiana na TBL mkoani Arusha wakipata maelezo ya kitaalamu katika mashamba yao ya Shahiri
mku5
Wakulima wanaoshirikiana na TBL mkoani Arusha wakipata maelezo ya kitaalamu katika mashamba yao ya Shahiri
………………………………………………………………………………….
*Mkakati huu kunufaisha maelfu ya wananchi kwa kuboresha maisha yao na kukuza wigo wa ajira
Kampuni ya TBL Group imeeleza kuwa pamoja na kuweka kipaumbele utekelezaji mkakati wa serikali wa  ukuzaji sekta ya viwanda nchini pia itaendelea kushirikiana na wakulima wanaozalisha malighafi kwa ajili ya viwanda vyake ili kuhakikisha sekta ya kilimo inakua na kutoa mchango katika  pato la taifa ikiwemo kuboresha maisha ya wakulima nchini.
Hadi kufikia sasa utekelezaji wa mpango wa kufanya kazi kwa kushirikiana na wakulima wadogo wadogo ambao umeanza kutekelezwa  na kampuni hiyo kwa wakulima wa zao la Shahiri kanda ya Kaskazini mwa Tanzania na wakulima wa Zabibu mkoani Dodoma umesaidia kuongeza ajira ikiwemo kuboresha maisha ya wakulima.
Mkurugenzi Mkuu wa  TBL Group ambaye pia ni Mkuu wa Masoko kanda ya Afrika Mashariki,Roberto Jarrin, amesema katika mahojiano maalumu,  kuwa mpango wa kilimo shirikishi unaotekelezwa katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro mbali na kuinua hali za maisha ya wakulima pia unanufaisha wananchi zaidi ya 3,000 wanaojipatia ajira katika utekelezaji wake na kwa upande wa zao la Zabibu zaidi ya wakulima  700  mkoani Dodoma wamenufaika.
Moja ya sera ya kampuni yetu ya “Dunia Maridhawa”-(Better World) inalenga kuwezesha wakulima katika maeneo tunayofanyia biashara zetu na kuwezesha jamii kuwa na  maendeleo endelevu katika shughuli za maisha yao ya kila  siku”.Alisema.
 
Aliyataja makundi ya wawaonufaika na mpango huu kuwa ni vibarua wanaofanya kazi mashambani kwa kupuliza dawa mashambani,madereva wa matrekta wanaolima mashamba na kuvuna,vibarua wa kupakia mazao na kuyashusha,wasafirishaji na watengenezaji na magunia ya kupakia mazao.
Alisema Mbali na wanaonufaika katika hatua  mbalimbali za utekelezaji wakulima wa zao la Shahiri katika mikoa ya Kaskazini ya Arusha na Kilimanjaro tayari  wameanza kuonja matunda ya ushirikiano huu kwa kuwa wanawezeshwa kuendesha kilimo cha kisasa,kupatiwa pembejeo,mbegu na wataalamu wa kutoa ushauri na wanakuwa na soko la uhakika kwa ajili ya kuuza mazao yao,hali ambayo imebadilisha hali zao za maisha kuwa bora.
“Mpango wa kampuni wa kushirikiana na wakulima haulengi kunufaisha wakulima wa Shahiri na Zabibu pekee bali pia wa mazao mengine kama mtama na mihogo na katika siku za usoni wakulima wa zao la mahindi watawezeshwa pia na wananchi  wengi watajipatia riziki kutokana na kufanya kazi za utekelezaji wake”.Alisema
Mpango huu wa kampuni kutegemea kupata malighafi kutoka  hapa nchini umeungwa mkono na serikali za nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania kwa kuwa unalenga kuinua hali za maisha za wananchi hasa wakulima ambao wana hali duni kutokana na changamoto nyingi zilizopo katika sekta ya kilimo.
Huu ni mfano wa uwekezaji wenye faida kwa watanzania kwa kuwa unaeleta mabadiliko kwenye jamii na kubadilisha maisha ya wananchi wengi kuwa bora.

No comments :

Post a Comment