Na Mahmoud Ahmad Kondoa
Mmiliki wa kampuni ya Kidee
Minning na polisi wilayani Kondoa wamekuwa wakiwakamata wachimbaji
wadogo na kuwabambikia kesi ili kuwatisha waondoke kwenye eneo la
machimbo ya dhahabu yaliopo kwenye Mtaa wa Tumbelo licha ya suala hilo
kuwepo kwenye mamlaka za
serikali wilayani humo.
Hadi sasa mmoja wa wachimbaji hao
anazuiliwa kituo cha polisi wilayani Kondoa huku akibambikiwa kesi ya
Madawa ya kulevya na polisi waliomkamata eneo la Kondoa mjini kwa madai
waliambiwa eneo hilo kunalimwa madawa ya kulevya hali hiyo imetokana na
wiki iliyopita kwa wachimbaji wawili kukamatwa.
Aidha imeonekana mmiliki wa
Kampuni hiyo amekuwa akiwatumia polisi kuendelea kuhakikisha anafanikiwa
kuwadhibiti wachimbaji hao na kulitwaa eneo wanalochimba madini ya
dhahabu katika Mtaa wa changaa licha ya suala hilo kuwapo kwenye mamlaka
za serikali zikishughulikia suala la leseni na mmiliki halali.
Sakata la Maombi ya Leseni kwa
wachimbaji wadogo wa madini kwenye eneo la Kata ya Changaa wilayani
Kondoa limegubikwa na sintofahamu kwa leseni kutolewa kinyume na
taratibu za utoaji wa leseni na kuwaacha waliomba leseni kwa mda mrefu.
Hatua hiyo imeonekana kwenye
Ofisi ya Madini Kanda ya Kati kutofika eneo la uchimbaji na kujiridhisha
ambapo kuna makundi matatu yaliomba leseni na kutoa kwa kampuni mmoja
bila kufuata taratibu hali inayoleta sintofaham kwa walikuwa eneo hilo
wakiendelea na uchimbaji
kwa kampuni ya kidee Minning hali
iliyopelekea wachimbaji na kampuni nyingine zilizotangulia kwenye
mchakato wa uombaji wa leseni kuachwa na kupewa kampuni hiyo.
Sakata hilo hadi sasa mamlaka
husika zimebakia na kigugumizi cha kuongea hatima ya wachimbaji wadogo
hao wenye kikundi cha KUMUCHA Changaa kinachotambuliwa na serikali ya
wilaya na huku wakiwa na pmo ya awali ya umiliki wa eneo hilo.
Akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake mkoani singida Kamishna msaidizi wa madini kanda ya
kati Sostenes Msola ameahidi kulifuatilia suala hilo kwa ukaribu ambapo
pia ataandikia ofisi yake iliyoko Dodoma kulifuatilia suala hilo.
Msola amesema kuwa licha ya ofisi
yake ya Dodoma kuonekana kutoa leseni bila ya kujiridhisha kufika eneo
la machimbo lakini kampuni hiyo ina leseni teyari hivyo ipo kisheria
japo kuna mazingira ambayo hayakuyafuata taratibu za kisheria.
Amesema kuwa suluhu ya jambo hilo
ni kukaa kwenye meza ya mazungumzo kulijadili kwa kuwaleta wote wenye
malalamiko mezani kwani hata hawa wachimbaji wadogo wana mashiko kwenye
suala hili kwani nia ya serikali ni kuona wachimbaji hao wanaendelezwa.
Nae Mmiliki wa Kampuni ya Kidee
minning Hassan Kidee alipotafutwa kwa njia ya simu kujibu tuhuma hizo
alidai yeye hana shida na wachimbaji hao wanaoendelea na uchimbaji na
waendelee na majukumu yao ila wafuate utaratibu wa uchimbaji.
Kidee amesema kuwa kijana
mchimbaji aliekamatwa na kwa kosa la kumtishia mwenyekiti wa serikali
ya mtaa wa tumbelo ila yeye alishiriki kuhakikisha kijana huyo
anapatikana ili kuondoa sifa mbaya kwa wachimbaji hao.
No comments :
Post a Comment