Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila akiwasilisha
mada: “Ardhi; Ufunguo wa Utawala Bora na Maendeleo ya Uchumi kwa
Tanzania”. Katika Mkutano wa 18 wa Benki ya Dunia wa masuala ya Ardhi na
Umaskini; Washington DC, Marekani.
Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila, akiwa
ameambatana na Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji;
Immaculate Senje, Kaimu Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya
; Amina Rashidi, wakijadili jambo na wajumbe wenzao wa Mkutano wa 18 wa
Benki ya Dunia wa masuala ya Ardhi na Umaskini; Washington DC, Marekani
Wajumbe kutoka Tanzania katika
picha ya pamoja na ujumbe kutoka Finland kwenye mkutano wa 18 wa Benki
ya Dunia kuhusu masuala ya Ardhi na Umaskini uliofanyika mjini Washington DC, Marekani
Wajumbe kutoka Tanzania wakifanya
mazungumzo ya pamoja na mtaalamu mwelekezi wa Benki ya Dunia kutoka
nchini Uganda; Bwn. Moses Kibirige (aliyevaa miwani) kwenye mkutano wa
18 wa Benki ya Dunia kuhusu masuala ya Ardhi na Umaskini uliofanyika
mjini Washington DC, Marekani
Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila, akiwa na
wajumbe wengine kutoka nchi mbalimbali katika vikao vinavyoendelea
katika Mkutano wa 18 wa Benki ya Dunia kuhusu masuala ya Ardhi na
Umaskini uliofanyika mjini Washington DC, Marekani
……………………………………………………………………….
Na Mboza Lwandiko
Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Imeshiriki Mkutano wa mwaka wa 18 wa Benki ya Dunia
unaohusu masuala ya Ardhi na Umaskini, Machi 20 – 24, 2017 – Washington
DC – Marekani.
Mkutano huo unaobeba ujumbe;
“Utawala bora wa Ardhi”, umejumuisha zaidi ya wajumbe 1,200 kutoka nchi
wanachama, zilizohusisha Serikali, taaluma, jamii na Sekta binafsi
mbalimbali.
Pamoja na mambo mengine; Mkutano
huo umejikita zaidi katika Maboresho mbalimbali yanayoendelea kufanyika
katika Sekta ya Ardhi Duniani, ikiwa ni pamoja na kuzingatia nafasi ya
takwimu na shuhuda zinazoashiria maboresho katika Sera za Ardhi, na
kuainisha Mikakati ya
Maendeleo katika kuboresha zaidi Sekta ya Ardhi.
Aidha, Mada ambayo imewasilishwa
na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imewasilishwa na
Katibu Mkuu wa Wizara; Dkt. Yamungu Kayandabila, ambayo ilibeba ujumbe –
“Ardhi; Ufunguo wa Utawala Bora na Maendeleo ya Uchumi kwa Tanzania”.
Alieleza kuwa utawala wa Ardhi Tanzania unazingatia; Sheria, Uwazi,
Uwajibikaji na Ushirikishwaji wa Wananchi. Pamoja na mengine Dkt.
Kayandabila alieleza jitihada mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanyika
kuboresha sekta ya ardhi nchini na juhudi ambazo zinaendelea kuboresha
utawala bora wa Ardhi nchini.
Baadhi ya maboresho aliyoyataja
ni pamoja na; Kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995, Upimaji wa
viwanja katika maeneo ya vijijini; mfano; Ulanga, Kilombero na Mvomero
(Morogoro) kwa mradi wa Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi (LTSP) na
uendeleaji wa kujenga mfumo unganishi wa taarifa za ardhi ujulikanao
kama Integrated Land Management Information System (ILMIS).
Wajumbe wengine waliohudhuria
Mkutano huo ni pamoja na; Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Mipango
na Matumizi ya Ardhi (NLUPC), Dkt. Stephen Nindi, Kamishna msaidizi wa
Ardhi, kanda ya Dar es Salaam; Mathew Nhone; Mkurugenzi msaidizi wa
Idara ya Mipango Miji na Vijiji; Immaculate Senje, Kaimu Msajili wa
Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya ; Amina Rashidi, wote wa Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mkurugenzi wa Manispaa ya
Kinondoni; Aaron Kagurumjuli na Afisa Ardhi wa Manispaa ya Kinondoni;
Rehema Mwinuka.
Aidha, ujumbe kutoka Tanzania
ulipata fursa ya kuonana na ujumbe wa Finland akiwemo aliyekuwa balozi
wa zamani wa Finland nchini Tanzania; Sinikka Antila, Mkurugenzi wa
upimaji na ramani wa Finland na wawakilishi wa makampuni mbalimbali ya
vifaa vya upimaji na ramani na softwares wa Master plans. Wajumbe hao walifikia makubaliano ya ujumbe wa Finland kufika Tanzania kwa mazungumzo zaidi.
Baadhi ya mada zilizowasilishwa
kwenye Mkutano huo ni; Jinsi utawala wa ardhi, unavyoongeza kodi ya
Mapato na kuwezesha upatikanaji wa Ajira, Worldbank, Uganda; Matumizi ya takwimu za ardhi kwa utawala wa Serikali za Mitaa. Location International;
UK ; Kuboresha Utawala wa Ardhi kwa Utawala Bora; Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Mijji, Uganda; Kuwezeshwa kwa Wananchi na
Matumizi ya Ardhi, maendeleo ya ardhi na utawala wa taasisi, Kenya; na
Uzoefu wa Sekta Binafsi katika sekta ya Ardhi- USAID, Marekani.
No comments :
Post a Comment