|
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO, ambaye pia ni
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, (wapili kulia), akipeana
mikono na Kaimu Meneja wa Uendeshaji wa BoT, tawi la Zanzibar,
Bi.Graceana Bemeye, muda mfuoi baada ya kufungwa kwa semina ya mafunzo
wka waandishi wa habari za Uchumi na Fedha, kwenye ukumbi wa BoT, tawi
la Zanzibar mjini Unguja, leo Machi 31, 2017. Wakwanza kushoto ni Kaimu
Meneja Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BoT, Bi. Vicky Msina. |
|
Dak.
Hassan Abbasi akizungumza wakati akiwasilisha mada juu ya Sheria mpya
ya Huduma za vyombo vya Habari wakati wa kufunga semina ya mafunzo kwa
waandishi wa habari za Uchumi na Fedha mjini Zanzibar |
Kaimu Meneja wa Uendeshaji wa Bot, tawi
la Zanzibar, Bi.Graceana Bemeye, (aliyesimama), akitoa hotuba ya kufunga
semina hiyo. Kulia ni Bi. Vicky Msina
|
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
MKURUGENZI
wa Idara ya Habari MAELEZO, ambaye pia ndiye Msemaji Mkuu wa Serikali,
Dkt. Hassan Abbasi, (pichani juu), ameipongeza Benki Kuu ya Tanzania,
(BoT), kwa kuandaa semina ya mafunzo kwa waandishi wa habari za Uchumi
na Fedha, iliyomalizika mjini Unguja, Zanzibar leo Machi 31, 2017.
Dkt.
Abaasi alisema, BoT, kama taasisi ya serikali inao wajibu wa kuwapatia
habari wananchi kupitia waandishi wa habari na uamuzi wa kutoa mafunzo
hayo ni ishara tosha ya ushirikishaji wa waandishi katika kuhakikisha
wananchi wanapatiwa habari sahihi kutoka BoT.
"Tumekutana
hapa wakati serikali imepitisha sheria mbili, moja ni ile inayohusu
huduma za vyombo vya habari, na ya pili ni ile ya haki ya waandishi
kupata taarifa kutoka taasisi za serikali na mimi nikiwa kama msimamizi
mkuu katika eneo hili la utoaji habari kwenye taasisi za umma,
ninawaalika mtusumbue sana katika kupata taarifa maana utoaji wa habari
kwa sasa si suala la utashi tena bali ni la kisheria." Alisema Dkt.
Abbassi.
Dkt. Abbasi pia aligusia wajibu wa waandishi wa habari katika kutekeleza majukumu yao chini ya sheria ya sasa,
“Lengo
la sheria hii ni kuwajengea heshima Waandishi wa habari ili waweze kufanya
shughuli zao katika mazingira ya heshima na bora, tofauti na hivi sasa ambapo
taaluma ya uandishi wa habari imekuwa ikilalamikiwa kwa kuchafuliwa na baadhi
ya waandishi ambao kimsingi hawana sifa za kuwa waandishi wa habari.” alisema na kuongeza,
“kila
taaluma, iwe taaluma ya Sheria, iwe taaluma ya udaktari, lazima wote walio
kwenye taaluma hizo wanasimamiwa na kanuni na sheria, kwa hivyo sheria hii itatenganisha kati ya waandishi wana taaluma na wale
ambao si wana taaluma.” Alisema.
Dkt.
Abbasi pia amekanusha habari kuwa Serikali kupitia sheria hii inataka kuwazuia
baadhi ya watu wasifanye kazi za uandishi kwa kigezo cha kitaaluma.
“Hii
si kweli, hata Yule anayeitwa Kanjanja,
anaweza kufanya kazi ya uandishi lakini kwa kuzingatia kanuni mpya
zinazoangazia sheria hii mpya, hivyo hata wale ambao si wanataaluma na
wanafanya kazi za kiuandishi wanayo fursa ya kufikia vigezo vya kuitwa
waandishi wa habari kwa mujibu wa kanuni hizo ambazo tayari zimeanza kufanya
kazi.” Alifafanua.
Aidha
Dkt. Abbasi amesema, Sheria hii ya sasa inatoa fursa kwa chombo cha habari
kuomba radhi na kuchapisha habari ambazo zina makosa kwa nia ya kuzisahihisha,
na swala hilo likakubaliwa kisheria na halitapelekwa mahakamani chini ya
kifungu cha 40 cha sheria ya Huduma za vyombo vya habari.
Akifunga maunzo hayo, Kaimu Meneja
Uendeshaji wa BoT tawi la Zanzibar, Bi. Graceana Bemeye aliwashukuru
waandishi hao kwa ushiriki wao uliotukuka. "Niwahakikishie kuwa BoT,
inatambua umuhimu wa waandishi wa habari katika shughuli zake za kila
siku, hivyo tutaendelea kutoa mafunzo haya ili kujenga uwezo wa
waandishi kuandika kwa usahihi habari zinazohusu BoT kwa manufaa ya
taifa.Aidha Kaimu Meneja Uhsuiano wa Umma na Itifaki wa BoT, Bi. Vicky
Msina, alisema mafunzo yaliyotolewa na BoT kwa waandishi hao wa habari
ni moja ya majukumu ya BoT katika kuelimisha umma na kwamba mafunzo hayo
yalijumuisha waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari vya Bara na
Zanzibar, vikiwemo vile vya kielektroniki, magazeti na Mitandao ya
Kijamii. "Lengo ni kuhakikisha tunawajengea uwezo waandishi wa habari za
Uchumi na Fedha ili waweze kuripoti kwa usahihi habari za BoT. "Lakini
pia BoT, kupitia website yake imeanza kutafsiri baadhi ya taarifa zake
kwa lugha ya Kiswahili ili kutoa wigo mpana kwa wananchi kuzielewa
taarifa za BoT." Alisema. Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa semina
hiyo, Bw. Ezekiel Kamwaga, aliishukuru BoT kwa kuandaa semina hiyo na
kuhimiza ushirikiano zaidi katika utoaji wa habari zinazohusu taasisi
hiyo nyeti hapa nchini. |
|
|
Kaimu Meneja Uhsuiano wa Umma na Itifaki wa BoT, Bi. Vicky Msina
Mwenyekiti wa Semina, Bw. Ezekiel Kamwaga, akizungumza
Afisa Uhusiano Mkuu kutoka Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BoT, Bw. Lwaga Mwambande
Baadhi ya wanasemina wakisikiliza hotuba
Maafisa wa BoT, Bw.Lusajo Mwankemwa, (kushoto), na Bi.Flora Mkemwa
|
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa
Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, (Kushoto), akipeana mikono na Mmiliki wa
K-VIS Blog, Bw. Khalfan Said mwishoni mwa semina hiyo |
|
Dkt. Abbasi akitoa semina |
Dkt. Abbasi (kushoto), akimsikiliza
Mchumi Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, BoT,
Bw.Lusajo Mwankemwa, wakati wa ufungaji wa semina hiyo
Mwandishi wa habari wa Sauti ya Ujerumani, (DW), mwenye makazi yake Zanzibar, Bi. Salma Said, akizungumza
Bi. Vicky Msina, (kushoto) na Bw. Lusajo Mwankemwa
Picha ya pamoja
No comments :
Post a Comment