Friday, March 31, 2017

MIAMALA YENYE THAMANI YA TRILIONI 5 KUPITIA MITANDAO YA SIMU HUFANYIKA KILA MWEZI: MTAALAMU WA BoT



NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MIAMALA yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania Trilioni 5 kupitia mitandao ya simu za mkononi (mobile payment service), hufanyika kila mwezi, Meneja wa Mifumo ya Malipo wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Bw.James Massoy amesema.
Akitoa mada ya Sheria Mpya ya Mifumo ya Malipo na Kanuni zake, kwenye semina ya wiki moja ya waandishi wa habari za Uchumi na Fedha, kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), tawi la Zanzibar Machi 30, 2017, Bw. Massoy pia alisema, kuna kadi za simu, (CIM Cards) Milioni 18 hapa chini ambazo zinafanya kazi (active).
Aidha akifafanua zaidi, Bw. Massoy alisema, huduma ya kufanya miamala ya simu imekuwa na faida kubwa sana kwa wananchi katika shughuli zao za kila siku na kueleza kuwa kwa mujibu wa taratibu na kanuni za BoT katka kufanya miamala kwenye simu, kiwango cha juu cha kuhamisha fedha kupitia simu, ni Shilingi Milioni 1,000,000/= kwa miamala ya kawaida ingawa sheria pia inatoa fursa kwa mwananchi yoyote kutegemea na shughuli zake, endapo atahitaji kufanya muamala wa kiwango kinachozidi Shilingi Milioni 1,000,000/= basi mteja huyo atatakiwa kuwasilisha nyaraka zake kwa mtoa huduma na mtoa huduma akijiridhisha na taarifa hizo za mteja basi anaruhusiwa kufanya muamala unaozidi Shilingi Milioni 1,000,000.
 Hata hivyo alisema, wateja wa mitandao ya simu wenye kuhitaji kufanya miamala kwa kutumia simu zao kwa kiwango kinachozidi Shlingi Milioni 1,000,000=,  wanaweza kuruhusiwa kufanya hivyo baada ya kuwasilisha nyaraka zenye maelezo yao kwa watoa huduma za simu hizo.
Akifafanua zaidi kuhusu Mifumo ya Malipo Tanzania, Muundo na Sheria zinazolinda Mifumo hiyo, Meneja Msaidizi Kurugenzi ya Mifumo ya Malipo, ya BoT, Bw. George Ben Sije, alisema, Mfumo huo tafsiri yake ni utaratibu wa kutoa fedha kutoka kwa mlipaji kwenda kwa mlipwaji, ingawa washiriki kwenye mfumo huo ni pamoja na Serikali, Benki Kuu, Watoa Huduma,(Mabenki), Watoa huduma ndogondogo,(Micro-finance) watoa huduma wezeshi,(maxcom, selcom) na Wateja.
Alisema, Mfumo wa Malipo uko katika hali (form) tatu ambazo ni pamoja na Malipo Taslimu,(Cash), Mfumo wa Digitali,(Ki-electroniki), Kadi za Malipo, (Payments Cards).

 Meneja Msaidizi Kurugenzi ya Mifumo ya Malipo, ya BoT, Bw. George Ben Sije
 Mwandishi wa The Citizen, Bi. Rose Mirondo, akiandika kilichokuwa kikifundishwa



No comments :

Post a Comment