Friday, March 24, 2017

SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA UWEKEZAJI KATIKA VIWANDA VIDOGO NA BIASHARA NDOGO

SEI
Katibu Mkuu Sekta ya Viwanda, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru akifungua warsha ya siku moja ya tathmini ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
SEI 1
 Katibu Mkuu Sekta ya Viwanda, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo Bw. Boniface Michael.
SEI 2
Mwenyekiti Asasi ya Mikono Cultural Heritage Bw. Henry Orauya akieleza jambo kwa Katibu Mkuu Sekta ya Viwanda, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru, mara baada ya ufunguzi wa  warsha ya tathmini ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo Bw. Boniface Michael.
SEI 3
Katibu Mkuu Sekta ya Viwanda, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa warsha ya tathmini ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
SEI 4
Mratibu wa Masuala ya Ukimwi nchini toka Shirika la Kazi Duniani (ILO) Bibi. Getrude Sima akisisitiza jambo kwa Katibu Mkuu Sekta ya Viwanda, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru mara baada ya ufunguzi wa warsha ya tathmini ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Frank Mvungi-MAELEZO)
……………..
Na Fatma Salum-MAELEZO
Serikali kupitia Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji inaendelea kufanya maboresho ya sekta ya viwanda ili kuendana na kasi ya ujenzi wa uchumi wa viwanda hapa nchini.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Sekta ya Viwanda, Wizara ya Viwanda Biashara na
Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru wakati akifungua warsha ya siku moja ya tathmini ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Meru alieleza kuwa lengo la kufanya tathmini hiyo ni kuboresha mazingira ya uwekezaji kwenye viwanda vidogo na vya kati kwa kuwa kuna mabadiliko mengi yamefanyika tangu sera hiyo ianze kutumika mwaka 2003.
“Viwanda hivyo vinachangia asilimia 27 ya pato la taifa hivyo ni muhimu kupitia upya sera hii na kupata maoni ya wadau kwani hivi sasa kuna mabadiliko mengi ya teknolojia, sheria na taratibu za uwekezaji.” Alisisitiza Dkt. Meru.
Aidha alisema kuwa Serikali itafungua dirisha dogo kwenye Benki ya Uwekezaji (TIB) kwa ajili ya kuwasaidia wawekezaji wa viwanda vidogo na vya kati kupata mitaji ya kuanzisha na kuendeleza viwanda vyao.
Akieleza mipango ya baadae Dkt. Meru alibainisha kuwa Serikali ina mpango wa kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Viwanda itakayowawezesha wazawa na wawekezaji wengine kupata mitaji yenye riba na masharti nafuu ili kuchochea ukuaji wa sekta hiyo.
Dkt. Meru alitoa wito kwa Watanzania kujikita kwenye uwekezaji wa viwanda kwa kuwa ndio njia pekee ya kukuza uchumi kwa haraka na kuongeza ajira, teknolojia, biashara na mitaji.
Tathmini ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda imekusudiwa kutoa mwelekeo wa namna bora ya kujikita kwenye uchumi wa viwanda kupitia uwekezaji wa viwanda vidogo na vya kati.

No comments :

Post a Comment