SAMATTA AJIUNGA NA WENZAKE TAIFA STARS KUWAVAA BOTSWANA NA BURUNDI thumb_IMG_2066_1024

Nahodha wa timu ya taifa Taifa
Stars,Mbwana Samata amewasili rasmi hapa nchini tayari kwa ajili ya
kujiunga na timu ya Taifa kujiandaa na michezo miwili ya kimataifa ya
kirafiki iliyo kwenye kalenda ya FIFA.
Baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julias
Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam mishale ya saa tisa usiku,Samata
amesema kwamba anajiunga na timu ya Taifa kwa lengo moja tu la kupigania
taifa lake ili lifanikiwe kufanya vizuri katika mechi hizo mbili.
Alisema kuwa licha ya kuonekana kwake kuwa ni mchezaji wa
kimataifa lakini amewataka watanzania kufahamu kuwa Samata ni yule yule
wa awali labda kilichobadilika kwa upande wake ni uzoefu katika
uchezaji.
Aidha alisema kwamba kwa sasa nguvu zao wanazielekeza kwenye
mechi hizo ili wapate ushindi wakiwa nyumbani na amewataka watanzania
kutofikilia swala la nafasi iliyopo Tanzania katika ubora wa viwango vya
FIFA.
Hata hivyo amedai kuwa licha kuwepo kwa mabadiliko kwenye benchi
la ufundi la timu hiyo linaloongozwa na kocha Salum Mayanga, ana imani
na kocha huyo kwani si mgeni katika timu hiyo ya Taifa Stars ingawa
kutakuwa na mabadiliko ya kiufundishaji kwani kila kocha ana mbinu zake.
Stars inataraji kushuka dimbani siku ya tarehe 25 ya mwezi huu
kumenyana na Botswana kisha kucheza mchezo mwingine wa pili na Burundi
utakaopigwa tarehe 28 ya mwezi huu,mechi zote mbili zikipigwa kwenye
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Shar
No comments :
Post a Comment