Mwenekiti wa halmashauri ya Mufindi akihitimisha warsha hiyo ya uzinduzi wa mradi wa vijana kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Iringa
Baadhi ya washiriki wakiwa katika halfa ya uzinduzi wa mradi huo wa vijana
Washiriki wakimsikiliza kwa makini mkuu wa mkoa wa Iringa hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa mradi huo
Frimina Kavishe kutoka mradi wa EAYIP akitoa ufafanuzi wa mradi huo |
wasanii wa kundi la muungano culture Troupe wakitoa burudani ya kizanzibar |
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akipokelewa katika ukumbi wa Siasa ni kilimo leo
Washiriki wakisikiliza kwa makini hotuba ya uzinduzi |
Wanahabari wa vyombo mbali mbali wakifuatilia uzinduzi wa mradi huo ambapo mkuu wa mkoa amewaomba kufuatilia kwa karibu mradi huo |
Katibu tawala wa wilaya ya Iringa akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha mkuu wa mkoa |
Baadhi ya viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa mkoa wa Iringa |
Mkuu wa mkoa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wawakilishi wa vijana |
Baadhi ya washiriki wa uzinduzi huo
Mkuu wa
mkoa wa Iringa Amina Masenza wa tatu kushoto waliokaa akiwa katika picha
ya pamoja na viongozi na washiriki wa uzinduzi wa mradi wa
ushirikishwaji vijana wa Afrika Mashariki katika sekta ya Kilimo na
mifugo
………………………………………………….
Na matukiodaimaBlog
SERIKALI
mkoani imepongeza jitihada za shirika la kimataifa la Heifer
International kwa kuanzisha Mradi rafiki kwa vijana Mardi
waushirikishwaji wa vijana Afrika Mashariki katika sekta ya Kilimo na
mifuko (EAYIP).
Huku
akitaka katibu tawala wa mkoa wa Iringa kuwawajibisha maofisa vijana wa
Kilolo na Mafinga mji kwa kushindwa kuwapa vijana kipaumbele cha
kushiriki uzinduzi huo.
Akizindua
Mradi huo leo katika ukimbi wa siasa ni kilimo mjini Iringa, mkuu huyo
wa mkoa alisema kuwa mradi huo umekuja wakati ambao vijana wengi
wanahitaji kuwezeshwa katika sekta ya kilimo na mifugo.
Mkuu huyo
wa mkoa alisema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi mzuri wa
Rais Dkt John Magufuli umedhamilia kuifanya Tanzania ya viwanda na
jitihada hizo zimeanza kuonekana na kuwa mradi huo utawezesha vijana
kunufaika na viwanda hivyo.
Hivyo
alisema njia pekee kwa vijana kupiga hatua ni kujikita katika vikundi
vya kiuchumi kwa kuanzisha kilimo na ufugaji na kwa kupitia mradi huo wa
EAYIP vijana wawe na uhakika wa kupiga hatua.
“Nimefurahi
sana kusikia ya kwamba shirika la Heifer International limeanzisha
mradi huu wa miaka mitano wa ushirikishwaji wa vijana katika kilimo na
mifugo lengo likiwa ni kuwezesha vijana wenye umri wa kati ya miaka 15
hadi 24 wapatao 10,453 nchini “
Alisema
kuwa kundi la vijana waliolengwa na mradi huo linakabiliwa na changamoto
nyingi sana lakini pia kundi hilo huwa linaachwa nyuma katika mambo
mengi sana kwani mara nyingi hujitoa kama hawana uwezo wa kushundania
fursa zinazojitokeza.
Masenza
alisema kuwa serikali inatarajia kuona mradi huo unawasaidia vijana
walengwa na kuwa wale wote watakaokwamisha mradi huo watawajibishwa.
Aidha
alisema katika mkoa wa Iringa wapo wawekezaji katika sekta ya kilimo na
mifugo hususani mazao ya mifugo kama vile maziwa kupitia kampuni ya Asas
na kwa upande wa kilimo wapo kiwanda cha kusindika nyanya cha Dabaga
hivyo viwanda hivyo ni fursa kwa vijana.
Japo
alisema viwanda vyote hivyo vinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa mali
ghafi na hivyo kupitia mradi huo vijana hawana budi kuongeza jitihada
kubwa.
Kaimu
meneja mkuu wa mradi huo Damas Damian alisema mradi huo utakuwa ni
mkombozi mkubwa kwa vijana na upo mikoa minne ambayo ni Iringa, Songwe,
Njombe na Mbeya.
Kuwa kwa
upande wa mkoa wa Iringa mradi huo uasimamiwa na shirika lisilo la
kiserikali linalojihudisha na maendeleo ya vijana la Restless
Development .
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Juma Masenza akizindua mradi wa wa ushirikishwaji vijana wa Afrika Mashariki katika sekta ya Kilimo na mifugo leo mkoani Iringa |
Kuwa kuna kuna fedha za kutosha kwa ajili ya kuwezesha mradi huo hivyo vijana.
No comments :
Post a Comment