Friday, March 24, 2017

MD KAYOMBO AKAGUA ENEO LITAKLOTUMIKA KWA AJILI YA MAONESHO YA NANENANE LA MANISPAA YA UBUNGO LILILOPO MKOANI MOROGORO


YOMBO
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea Shamba litakaloandaliwa kwa ajili ya Maonesho ya Nanenane lililopo Mkoani Morogoro
 


Na Mathias Canal, Morogoro
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amefanya
ukaguzi wa eneo kwa ajili ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) ili
kujiridhisha na kutoa maelekezo ya maandalizi kwa kufyeka majani
yaliyopo katika eneo la JKT Mtaa wa Nanenane ikiwa ni hatua za ufanisi

kwa ajili ya kuelekea Maonesho ya Nane Nane mwanzoni kwa mwezi Agosti.
Kayombo amesema kuwa lengo kuu la kuzuru kwanza ilikuwa ni kujionea
eneo hilo sambamba na kuona hali ya utendaji kazi ili kuanza ufyekaji na
kuanza kulima mazao ambayo yanakusudiwa kuoneshwa na Manispaa ya
Ubungo.
Amesema kuwa katika utendaji wake amekusudia kwenda
mwenyewe Field ili kuona hali ya utendaji ilivyo sio kupelekewa Taarifa
pekee kwani kufanya hivyo Ukurugenzi alionao utakuwa hauna maana kama
ataishia ofisini.
“Rais ametupa mamlaka makubwa ya kuwatumikia
wananchi sasa kama tunakaa ofisi pekee nchi haiwezi kusonga mbele badala
yake ili tuweze kuwa na mafanikio katika utendaji pamoja na Kukuza
uchumi kupitia sekta mbalimbali ni wazi kwamba tunapaswa kuzuru katika
maeneo yote tunayoyaongoza” Alisema Kayombo
MD Kayombo amewapa
maelekezo Afisa Kilimo na Afisa Mifugo na Uvuvi kuanza haraka
iwezekanavyo usafishaji wa shamba hilo lenye ukubwa wa Mita za Mraba
3600 ili kulima na kupanda mazao kusudiwa kwa ajili ya Maonesho ya
Kilimo Nane Nane.
Maelekezo mengine ni pamoja na kununua
viuatilifu kwa ajili ya kuua wadudu waharibifu na magonjwa, kuandaa
mabango na kuainisha aina mbalimbali za malisho iliyooteshwa na kujenga
bwawa la samaki.
Kayombo alisema kuwa eneo hilo limenunuliwa na
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa ajili ya Maonesho ya Nane Nane
ambayo hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuwakutanisha wakulima,
Wafugaji na wavuvi kwa kuwaelimisha na kuwajengea uwezo wa kutumia
teknolojia na mbinu za kuongeza uzalishaji katika eneo la Uvuvi, Kilimo
na Ufugaji.
Akizungumzia utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa
na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Kaimu Afisa Kilimo wa Manispaa ya
hiyo Ndg Salim Msuya amesema kuwa wanataraji kuanza kutekeleza hivi
karibuni ikiwa ni pamoja na kujenga mabanda ya mifugo na sehemu za
kusindika mazao ya mifugo, kuandaa mavazi rasmi kwa ajili ya washiriki
wa Maonesho.
Mengine ni kukusanya bidhaa za mazao mbalimbali ya
wafugaji, wakulima na wavuvi watakaoshiriki Maonesho hayo ya Kilimo
Nane Nane kwa ajili ya kuyapeleka Morogoro.
Sambamba na hayo pia
Msuya amesema kuwa maandalizi mengine itakuwa ni kutengeneza matuta ya
kuoteshea malisho, Kununua mbolea na kuweka kwenye eneo la malisho ya
mifugo, kufunga maji katika eneo la malisho yatakayotumika kwa ajili ya
umwagiliaji na mifugo itakayopelekwa wakati wa Maonesho.
Msuya
ameeleza kuwa maandalizi mengine itakuwa ni kuandaa mashimo katika
matuta ya kuotesha miche, Vipande na Mbegu za malisho pamoja na
kutayarisha eneo la kwa kusafisha eneolima na kufanya Layout ya eneo la
kuchimba bwawa kwa ajili ya ufugaji samaki.

No comments :

Post a Comment