Friday, March 24, 2017

MBUNGE WA JIMBO LA CHALINZE ATAKA MAJIBU YA KURIDHISHA KUHUSU MRADI WA MAJI JIMBONI HUMO


ridhi
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete (CCM) amesema  Mradi  wa Maji ambao ulitakiwa kukabidhiwa mwezi huu jimboni humo umekwama.
Alisema hadi sasa hakuna matenki yaliyojengwa na pia  mabomba hayajafukiwa hivyo mradi huo hauwezi kukamilika mwezi huu.
 Ridhiwani amesema vikao vya bunge vikianza anahitaji waziri mwenye dhamana kueleza fedha za maji zilizopelekwa Chalinze pia kujua mradi unaisha lini.
“Wananchi wangu  wamechoka kusubiria maji ya matumaini wanahitaji maji nasio tena maneno hivyo bunge hili nitaomba waziri anipe majibu ya kueleweka “alisema Ridhiwani

No comments :

Post a Comment