Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo (
kulia) na Mkuu wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Canada, Sue
Steffen,(kushoto) akizungumza wakati wa mafunzo ya kufunga wa migodi
yanayotolewa kwa Kamati ya Kitaifa ya ufungaji Migodi.Mafunzo hayo ya
siku tano yanatolewa na Serikali ya Canada jijini Dar Es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo (
katika waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Kitaifa ya
ufungaji Migodi wakati wa mafunzo ya ufungaji wa migodi yanayotolewa
kwa siku tano jijini Dar es salaam na Serikali ya Canada. Kushoto kwake
ni Mkuu wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Canada, Sue Steffen, na kulia
kwake ni Afisa Rasilimali Watu Mkuu kutoka Wizara ya Nishati na Madini,
Suzan Kiwelu.
Washiriki wa mafunzo ya ufungaji
migodi ambao ni Kamati ya Kitaifa ya ufungaji Migodi wakifatilia mada
mbalimbali wakati wa mafunzo hayo yanayotolewa kwa siku tano jijini Dar
es salaam na Serikali ya Canada.
Afisa Rasilimali Watu Mkuu kutoka
Wizara ya Nishati na Madini, Suzan Kiwelu ( kulia) na Kaimu Kamishna wa
Madini, Mhandisi John Shija( kushoto) wakifuatilia mada wakati wa
mafunzo hayo yanayotolewa kwa siku tano jijini Dar es salaam na Serikali
ya Canada.
Wakufunzi wa mafunzo ya ufungaji
migodi kutoka nchini Canada wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo (
hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
………………..
Na Zuena Msuya DSM,
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini, anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo
amefungua mafunzo ya ufungaji wa migodi yanayotolewa kwa wataalam wa
mbalimbali wanaoshiriki katika Kamati ya Kitaifa ya ufungaji wa Migodi.
Watalaam hao wanatoka katika
Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali, lengo likiwa ni kuwajengea
uwezo wa kukabiliana na changamoto zinazojitokeza wakati wa ufungaji wa
migodi nchini.Mafunzo hayo yanatolewa jijini Dar Es Salaam,na Serikali
ya Canada kwa siku tano kuanzia 27-31 machi 2017.
Akizungumza wakati wa akifungua wa
mafunzo hayo, Dkt. Pallangyo alisema kuwa mafunzo hayo yatawawezesha
wataalamu wa migodi nchini kuwa na uelewa zaidi juu ya hatua zote
zinazotakiwa kufuatwa wakati na baada ya ufungaji wa migodi ili kuondoa
changamoto mbalimbali zilizokuwa zikijitokeza baada ya migodi kufungwa.
Dkt. Pallangyo, alifafanua kuwa,
kwakuwa Serikali ya Canada imejikita katika Sekta ya Madini kwa zaidi ya
miaka 200, hivyo mafunzo hayo yatawasaidia wataalam wa ndani kufahamu
na kujifunza namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali
zinazojitokeza kupitia migodi iliyokwishafungwa katika nchi hiyo ili
yasijitokeze hapa nchini.
” Tusiwe watu wa kusoma tu na
kufunga migodi, tujifunze kwa vitendo kutoka kwao makosa waliofanya
wakati wa ufungaji wa migodi kwa kuwa Canada ipo katika Sekta ya madini
kwa zaidi ya miaka 200 na tujirekebishe, ili makosa yaliyotokea kwa
yasijirudie katika migodi yetu,” alisisitiza Dkt.Pallangyo.
Vilevile, ameiomba Serikali ya
Canada kutoa mafunzo hayo mara kwa mara na kwa muda mrefu ili kupata
wataalam wengi zaidi na wenye uelewa mpana katika Sekta ya Madini hasa
ufungaji wa migodi hapa nchini: Mafunzo hayo yatawawezesha watalaam
kubaini kodi halisi inachotakiwa kulipwa Serikalini pamoja na njia
rahisi ya utunzaji wa ardhi na mazingira kwa ujumla.
Kwa upande wake, Mkuu wa Maendeleo
kutoka Ubalozi wa Canada, Sue Steffen aliesema kuwa nchi yake inauzoefu
wa zaidi ya miaka 200 katika sekta ya madini, hivyo wameona ni busara
kutoa mafunzo hayo kwa nchi zinazoendelea na zinazochimba madini
mbalimbali.
Alisema, lengo ni kutoa elimu na
kuzijengea uwezo wa kukabiliana na changamoto zilizowahi kujitokeza
katika ufungaji wa migodi nchini Canada, na hivyo kuziepusha nchi hizo
katika madhara yanayoweza kujitokeza.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo
hayo, Mhandisi Elizabert Nkini alisema kuwa mafunzo hayo yatawaongezea
uelewa zaidi katika ufungaji wa migodi, licha kuwepo kwa vigezo vya
ufungaji wa migodi hiyo lakini uelewa umekuwa ni mdogo kutokana
kutofahamu kwa vitendo changamoto nyingi.
“Migodi nchini ni muhimili mkubwa
wa mapato, lakini pia ni chanzo kikubwa cha uharibu wa mazingira, hivyo
kama mazingira na ardhi yetu havitatunzwa vizuri kabla na baada ya
kuchimbwa tutaicha nchi yetu katika hali ya jangwa isiyofaa na vyanzo
vya maji vitaharibiwa, hivyo mafunzo hayo yatatuwekea utatatibu mzuri wa
kuacha mazingira yetu yakiwa salama na ardhi salama pia,”. alisema
Mhandisi Nkini.
Aidha alisema kuwa elimu hiyo
waliyoipata wataifikisha kwa wananchi wanaozunguka Migodi husika ili na
wao wawe na uelewa juu ya ufungaji wa migodi kwa kufahamu taratibu na
hatua mbalimbali za kufuata kwa maslahi yao na taifa kwa ujumla.
No comments :
Post a Comment