Friday, March 24, 2017

KIKAO CHA KAMATI MAALUM ZANZIBAR CHAFANYIKA


ZAM1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Juma Abdalla Juma (Mabodi) alipowasili katika viwanja vya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar alipohudhuria katika Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 24/03/2017.
ZAM2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi  alipowasili katika viwanja vya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar alipohudhuria katika Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 24/03/2017. 
ZAM3
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakipitia mada mbali mbali za Kikao kabla ya kufanyika katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo,[Picha na Ikulu.] 24/03/2017.
ZAM4
Wajumbe wa kikao cha Siku moja cha Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakiwa katika  Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar leo kabla ya kuanza kwa kikao hicho mwenyekiti wake akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) [Picha na Ikulu.] 24/03/2017.
ZAM5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein(kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Juma Abdalla Juma (katikati) pamoja na Viongozi wengine   wakiwa katika Ukumbi wa Ofisi ya  CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar  katika Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar,[Picha  na Ikulu.]24/03/2017.
ZAM6
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein  (kushoto) akiteta na  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Juma Abdalla Juma   katika Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar
ZAM8
………………………………………………………………………
 Na Is-haka Omar, Zanzibar.
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, leo (jana) amekiongoza kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa..
Kwa mujibu wa  taarifa kwa vyombo vya Habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya
Halmashauri Kuu ya CCM wa Idara ya Itikadi na Uenezi Bi. Waride Bakari Jabu, amesema kikao hicho cha siku moja kilifanyika Afisi Kuu ya CCM, Mjini Unguja.
Ameeleza kwamba pamoja na mambo mengine, kikao kilipokea na kujadili majina ya wana CCM waliojitokeza kuomba ridhaa ya Chama hicho, ili waweze kuwania nafasi ya Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki, kwa kipindi cha mwaka 2017 – 2022.
“ Kutokana na Chama chetu kuwa Kinara wa Demokrasia  wanachama wengi wamejitokeza kuwania nafasi hizo ili waweze kuiwakilisha vyema CCM na serikali inazoziongoza katika Bunge hilo muhimu
Pia  Wana CCM na wananchi kwa ujumla tukumbuke kuwa fursa hizi zisingeweza kujitokeza kama nchi yetu ingekuwa katika mashaka na migogoro, hivyo wito wangu tuendelee kuwa wamoja ili wenzetu waweze kutuwakilisha vyema.”, alisema Bi. Waride.
Kikao hicho kimefanyika kwa kuzingatia Ibara ya 114 (7) (b) ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977, Toleo la  2012, ambayo inatoa Mamlaka kwa Kamati Maalum ya H/Kuu yaTaifa ya CCM Zanzibar, kupokea na kujadili na hatimaye kutoa mapendekezo yake kwa Kamati Kuu, kwa hatua zinazofuatia.
Bi. Waride amesema  jumla ya wana CCM 33, wakiwemo wanawake 7 na wanaume 26, kutoka Mikoa mbali mbali ya Unguja na Pemba, wamejitokeza kuomba  waruhusiwe na CCM kugombea nafasi hizo.
Katibu huyo wa Kamati Maalum ya NEC wa Idara ya Itikadi na Uenezi amefafanua kuwa kwa mujibu wa Katiba ya  Jumuiya ya Afrika Mashariki, Tanzania inapaswa kuwakilishwa na Wabunge  tisa (9).
Aidha kikao hicho kilimtambulisha Ndugu. Abdullah Juma Saadalla (Mabodi) aliyepitishwa na Mkutano Mkuu wa CCM hapo Machi 13, mwaka huu, kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar. Aidha, kimeahidi kumpa kila aina ya mashirikiano ili aweze kutekeleza majukumu yake aliyopewa na Chama  ipasavyo.
Hata hivyo Kikao pia kimewapongeza kwa dhati wana CCM hasa Vijana  waliojitokeza kuomba kugombea nafasi hizo muhimu za Uongozi katika  Jumuiya ya Afrika Mashariki hali inayoonyesha kuimarika kwa Demokrasia ndani ya Chama hicho.

No comments :

Post a Comment