Mkuu
wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akipata maelezo ya kasi ya upimaji VVU
leo Mufindi kwenye kilele cha siku ya kifua kikuu na UKIMWI
mkuu wa mkoa akiwa banda la benki ya wananchi wa Mufindi |
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akimkabidhi baiskeli zilizotolewa na Africare mtoa huduma majumbani Shukuru Ngelime leo
Na MatukiodaimaBlog
WAKATI Leo ni maadhimisho ya siku ya kifua kikuu Dunia imeelezwa kuwa kati ya watu 3447 waliojitokeza kupima afya zao wilaya Mufimdi mkoani Iringa idadi ya watu 27 wahisiwa kuwa na maambukizi ya kifua kikuu.
Akitoa
taarifa ya upimaji wa VVU na kifua kikuu leo wakati wa kilele cha
maadhimisho hayo yaliyofanyika kimkoa kwenye viwanja vya mashujaa mjini
Mafinga wilayani Mufindi mratibu wa Kifua kikuu na Ukimwi Mkoa Tecla
Orio,alisema idadi hiyo imetokana na wale waliojitokeza kupima kwa hiari
afya zao.
Alisema kuwa kwa wakati wote ndani ya wiki Moja sasa wamekuwa wakizunguka kata mbali mbali kupima kifua kikuu na Ukimwi.
“Tulifanya
kampeni ya huduma shirikishi ya ushauri nasaha na upimaji wa VVU,
uchunguzi wa wagonjwa wa shinikizo la damu pamoja na huduma ya uzazi wa
mpango”
Kuwa
jumla ya wanawake 2019 na wanaume 1368 ndio waliopima Ukimwi na kifua
kikuu na waliokutwa na maambukizi ya Ukimwi ni 49 wanawake ni 31 na
wanaume 18 wakati waliohisiwa kuwa na kifua kikuu ni wanaume 12 na
wanawake 15.
mratibu
huyo aliena kwa upande wa shinikizo la damu kati ya watu hao waliopima
kupitia kampeni hiyo ambao ni 655 walioonekana na shinikizo la damu ni
watu 191 wakiwemo wanaume 85 na wanawake 106.
Kuhusu huduma ya uzazi wa mpango waliochunguzwa 139 na wanawake 139 walipatiwa huduma ya kansa ya mlango wa uzazi.
Akiwahutubia
wananchi hao mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza aliagiza wakurugenzi
na wakuu wa wilaya zote mkoani Iringa kuanzisha utaratibu wa kuanzisha
mikusanyiko ya utoaji wa elimu juu ya afya.
Kuwa
wapo baadhi ya watu ambao wanauelewa ndogo juu ya kifua kikuu hivyo
kupitia mikusanyiko hiyo wataweza kupatiwa elimu sahihi na
wanapodungulika basi kuanzishiwa tiba.
Alisema
katika mkoa wa Iringa taarifa zilizopo ni zaidi ya wagonjwa 1000 ambao
hughundulika kila mwaka kati yao asilimia 40 wanayo maambukizi ya VVU.
Hivyo
aliwataka wananchi wakihisi kuwa na dalili za kifua kikuu kukimbilia
hospitali ili kuanzishiwa matibabu na moja kati ya dalili za kifua kikuu
mwili kupatwa joto Kali hata wakati wa baridi kali.
mkuu
huyo wa mkoa alitaja makundi ambayo yapo hatarini kupatwa na Kifua
kikuu kuwa ni watu wanaoishi na VVU, watu walio katika msongamano, wazee
zaidi ya miaka 65,watoto chini ya miaka mitano, watu wenye magonjwa ya
muda mrefu kama kisukari, saratani na mengine
Pia watu wenye lishe duni na walevi wa kupindukia hivyo kuwataka wananchi kupima afya zao
Wakati
huo huo mkuu wa mkoa amekabidhi jumla ya baiskeli 125 zenye thamani ya
shilingi milioni 18.7 kwa watoa huduma wa afya majumbani.
Mratibu
wa shirika la Africare G. Fund Aloyce Mkangaa alisema baiskeli hizo
zimetolewa kwa wahudumu wa wilaya ya Mufindi na Iringa.
No comments :
Post a Comment